Saturday, January 18, 2014

LIGI YA MBUZI YAENDELEA TEKU

Ligi ya mbuzi inayofanyika katika chuo kikuu cha Teofilo Kisanji kilichopo jijini Mbeya imeendelea leo kwa kushuhudiwa mpambano mmoja kati ya timu ya BASO  na BAED.

Timu hizo zimetoka kwa kutoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1, magoli ambayo yote yalifungwa kwa shuti kali inje ya eneo la hatari.

Ilikuwa ni kipindi cha kwanza ambapo winger wa timu ya BASO Joseph Siwingwa alipo wanyenyua washabiki kwa kufumua shuti kali baada ya kupokea pasi murwa kutoka kwa Sanga Festor.

hizi ni baadhi ya picha wakati wa mtinange huo.


Wachezaji wa Baso wakipata maji kipindi cha mapumziko.