mmoja wa waliochanngia hoja Siwingwa Josephat akiongea kwa msisitizo.
WANAFUNZI wa
mwaka wa pili (BASO) katika chuo kikuu cha Teofilo kisanji university kilichopo
nyanda za juu kusini mkoani Mbeya leo wamefanya kikao ili kujadili mambo mbali
mbali katika chuo chao.
Akifungua kikao hicho mbunge wa BASO mwaka wa pili mh. Tweve
Nehemia alianza kwa kuwapongeza wote waliofanikiwa kuhudhuria kikao hicho na
hatimae kusoma ajenda mbalimbali. Tweve alizitaja ajenda hizo kuwa ni; mwenendo
wa mfuko ulionzashwa na wanafunzi wa BASO ilikuwasaidia pale matatizo
mbalimbali yanapo jitokeza, ushiriki wa wanafunzi katika shughuri za kitaaluma
na mwisho namana ya kusaidiana katika taaluma na michango ya kufiwa na pongezi
pale mmoja wao anapojifungua
Tweve aliwashukuru sana
walio kabidhiwa dhamana ya kuhakikisha mfuko huo (TEKUBA) unaendelea vizuri mh.
Paul Edward na Ng’ahara Zaina kwa kutekeleza jukumu lao ipasavyo.
Wakichangia ajenda ya ushirikiano katika suala la kitaalum
wengi walionekana wakiwalaum baadhi ya wenzao kutoshiriki vyema katika kazi za
makundi maarufu kama Group Assignment hali inayopelekea kuwapa kazi wenzao
ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu, hoja iliyo changiwa na Siwingwa Josephat, Castory, Nzunda Enock,
Bikombo Fidelis, Chiwambo Ausi, Ally Karafuu, Mandela Mselu, sun na kumaliziwa kwa msisitizo na Masunga Elikana.
Pia ajenda ya michango ya kufiwa na pongezi pale mmoja wao
anapojifungua zilishika kasi huku ikiamriwa kuwa mchango utakuwa kwa atakaye
fiwa tuu ndio utakuwa wa lazima na ule wa pongezi utakuwa hiari pale mtu mmoja
mmoja atakapo jisikia na aina yoyote ya zawadi atakayo kuwa na uwezo nayo
Mwisho mbunge wa
jimbo hilo Mh.
Tweve aliahirisha kikao kwa kuwataka wanabaso kuwa na ushirikiano katika mambo
mbali mbali hususani ya kiataaluma na kuwatakia sherehe njema za krismas na
mwaka mpya kwa kuwataka wanaondoka salama na waludi salama.
|
No comments:
Post a Comment