Wednesday, November 20, 2013

WAFUGAJI WAZUA BARA MBARALI

FAMILIA moja katika kijiji cha Utulo wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya imepata ulemavu wa viungo baada ya kudaiwa kupigwa na kujeruhiwa na wafugaji jamii ya kisukuma.

Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mmoja wa wahanga aliyefahamika kwa jina la Luchina Mgaya(55) mkazi wa kijiji cha Utulo alisema wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu baada ya kupata ulemavu hivyo kushindwa kujitafutia riziki.


FAMILIA moja katika kijiji cha Utulo wilaya ya Mbarali Mkoani hapa imepata ulemavu wa viungo baada ya kudaiwa kupigwa na kujeruhiwa na wafugaji jamii ya kisukuma.

Tukio hilo la kusikitisha liliikumba familia hiyo Januari Mwaka huu baada ya baba, Mama na mtoto kupata ulemavu baada ya kukosa matibabu yaliyotokana na kukosa msaada wa fedha kutoka kwa wanaotuhumiwa kutyenda kosa hilo.

Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mmoja wa wahanga aliyefahamika kwa jina la Luchina Mgaya(55) mkazi wa kijiji cha Utulo alisema wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu baada ya kupata ulemavu hivyo kushindwa kujitafutia riziki.

Luchina amesema alipigwa na wafugaji hao mapema mwaka huu baada ya mwanae wa kiume kuvamiwa na wafugaji hao wakidai kuwa aliwachongea kwenye uongozi wa kijiji hali iliyopelekea kukamatwa.

Alisema Baada ya kuona mwanae anapigwa mama huyo alifanya jitihada za kumuokoa ili asipate kipigo ndipo walipomgeukia na kumpa kipigo kikali yeye na mumewe ambapo yeye amepata ulemavu wa viungo na mumewe akiwa amepata upofu.

Luchina ametabanaisha kuwa baada ya kipigo kikali walitoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji na Polisi Rujewa ambapo watuhumiwa walikamatwa na kufunguliwa kesi lakini wakaomba kesi hiyo waimalize nje ya mahakama jambo ambalo walikubaliana nalo.

Aliongeza kuwa Pamoja na kukubaliana suala hilo kulimaliza nje ya mahakama ambapo watuhumiwa walikiri kutenda kosa na kuahidi kulipa jumla ya shilingi laki tano ikiwa ni gharama za matibabu na shilingi milioni nne ambazo ni fidia waliahidi kulipa kwa muda wa siku mbili tu.

Mhanga huyo alisema kitu cha kushangaza ni kitendo kilichofanywa na  watu waliopewa dhamana ya kutunza amani na sheria ambao ni Mwenyekiti wa kijiji na Askari mpelezi wa kesi hiyo kuzitafuna pesa hizo na kuwaacha wahanga hawana kitu mpaka leo.

Hata hivyo baadhi ya wanaotuhumiwa kuwazunguka wahanga hao walipotafutwa kuthibitisha kutenda kosa hilo waligoma kulizumzia kwa kile walichodai hawalijui kabisa.

Aidha familia ya Luchina imekuwa ikiishi maisha ya ombaomba, pamoja na kufukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi kwa kukosa pesa  za kulipa pango la nyumba na watoto watatu wameacha masomo kutokana na kukosa ada.

Wahanga hao wameziomba taasisi mbalimbali kuwasaidia ili waweze kupata haki zao kwani wamejitahidi kufuatilia maeneo yote lakini wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tamaa na wao kukata tama ya kuishi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amekili kupata taarifa za tukio hilo na kuahidi kulifuatilia na kulipatia ufumbuzi ndani ya mfupi na kuongeza kuwa watakaobainika kutenda kosa hilo la kinyama watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Vitendo vya unyanyasaji na ugomvi baina ya wafugaji na wakulima vimeendelea kuripotiwa katika maeneo mengi hapa nchini, hivyo lisipoangaliwa na kuchukuliwa kwa hatua stahiki amani ya Watanzania itakuwa matatani.

Tuesday, November 19, 2013

Rais Kikwete awasili Poland kwa ajili ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili jijini Warsaw, Poland, kuhudhuria mkutano wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Kyoto kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi unaoanza leo Jumanne Novemba 19, 2013. (picha hii na zinazofuata hapo chini zimetoka Ikulu)