Wednesday, February 13, 2013

KIGOMA ALL STARS WALA SHAVU LA KUWA MABALOZI WA NSSF

#InstaConference #Arusha #AICCR #AsNSSFFambassador #KiCorporateZaidi #KiNSSFzaidi #Mipango na #MaendeleoZaidi #kiCommunity na #Member wenzangu toka #LekaDutigiteCompany
Leo hii ikiwa ni dakika 30 zilizopita, kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na Banana , Mwasiti na wengineo wanaounda kundi la Kigoma All Stars, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Arusha AICC. Kutokana na maelezo aliyoyaandika chini ya picha hii, ni dhahiri kuwa wamekula shavu la kuwa mabalozi wa NSSF.
 Kama unakumbuka siku chache zilizopita, tulikuwekea picha hii ya tangazo la NSSF likiwa na picha za wasanii hao ya wasanii hao

MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO ...

Mbeya Yetu: MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO ...: BARAKA KIBONA, MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU HAPA AKIWA ND...

Monday, February 11, 2013

Mwanafunzi auawa,anyofolewa viungo

MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya Msingi Kasumulu, Kata ya Ngana, wilayani Kyela, Kaselema Mpale (14) ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali, kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyake sehemu ya mwili.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucia Kamnyonge alisema tukio hilo lilitokea Februari 8, mwaka huu saa 1:30 usiku, alipotumwa na baba yake kwenda nyumba ya jirani kuchukua mpunga ambao ungetumika kwa chakula usiku.
Kamnyonge alisema mtoto wake hakupatikanika hadi alipokutwa siku ya pili yake, akiwa amechinjwa na kunyofolewa baadhi ya sehemu zake za mwili ambazo ni pua, mdomo, jicho, kuondolewa sehemu zake za siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na utosi na mwili wake kutundikwa juu ya mti.
Aliendelea kuwa baada ya hali hiyo taarifa ilipelekwa ofisi ya serikali ya kijiji, uliitishwa mkutano wa wananchi wote na walitawanyika kuanza kumtafuta mtoto huyo bila ya mafanikio.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ibungumbati lilipotokea tukio hilo, Adam Mkese alidai tukio hilo limewashtua na kwamba, mkutano wa kijiji ulioitishwa kwa dharura wananchi walimhusisha baba mzazi wa mtoto huyo na mauaji hayo.
Mkese alidai watu wa kijiji hicho walimhusisha kutokana na mazingira tata ya kifo chenyewe na maelezo ya kujichanganya aliyoyatoa.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Naomi Charles alidai kuna dalili za mzazi huyo kuhusishwa na mauaji hayo na kwamba, polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Baruti Mwakasala alidai kuwa hali katika kijiji hicho siyo nzuri na kushukuru polisi kwa hatua za haraka walizochukua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alithibiti
sha kutokea kwa mauaji hayo na kukiri kumshikilia baba mzazi wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi.

Waziri ataka makahaba wapewe vitambulisho

WAZIRI wa Haki nchini Senegal, Aminiata Toure, amependekeza makahaba wote nchini humo wapewe vitambulisho maalum.
Matamshi yake yalitolewa huku nchi hiyo ikijiandaa kwa kongamano muhimu wiki ijayo kuhusu sheria za ukahaba.
Toure alisisitiza kuwa kadi hizo zipewe tu wanadada waliozidi miaka 18, na watakaokiuka hilo wakamatwe na kushtakiwa.
Vitambulisho vimekuwa vikitolewa bila malipo kwa makahaba tangu miaka 20 iliyopita lakini kwa machangudoa wanaoendesha biashara yao mjini Dakar na mitaa viungani.
Waliopewa kadi hizo walichunguzwa vikali na walihitaji kila mwezi kupita kipimo cha HIV/Ukimwi ama maambukizi mengine ya zinaa.
Waliokuwa wanaishi bila maradhi walitakiwa kutoa damu iliyowekwa katika hifadhi na kupewa hospitali.
Waliopatikana na maambukizi madogo walitibiwa na kuruhusiwa kwenda, na waliopatikana kuwa na vijidudu vya maambukizi walitengwa kando.
Juhudi hizo za tangu miaka ya mapema ya themanini kuhamasisha umma kuhusu janga la ukimwi, zinaaminika kupelekea Senegal kuwa miongoni mwa mataifa yaliyo na kiwango cha chini sana cha maambukizi ya HIV barani Afrika.
Kikosi maalum
Lakini kongamano hilo la Jumatano linanuia kung’oa watoto katika biashara hiyo
na kuweka msingi wa sheria zenye uhalisi, kali na thabiti na mikakati ya kudhibiti ukahaba nchini Senegal.
Waziri huyo pia alipendekeza kikosi maalum kilichoundwa kuwafuatilia mahakaba kipewe vifaa vya kutosha na vizuri vya kuwawezesha kutekeleza jukumu hilo.
“Ili kudhibiti vyema ukahaba nchini Senegal, twahitaji ushirikiano wa wadau kadha kama viongozi wa kidini na muhimu zaidi wadau katika sekta ya utalii na burudani.”

Wagombea Urais Kenya Kupambana Katika Mdahalo

WAGOMBEA urais nchini Kenya wanatarajia kuumana katika mdahalo utakaowakutanisha viongozi hao na kuoneshwa moja kwa moja kupitia runinga. Mdahalo huo ambao ni wa kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo na unaotarajiwa kupima uwezo wa wagombea hao juu ya masuala muhimu ya kitaifa unafanyika wakati joto la kampeni likiwa juu hivi sasa.

Mjadala huo ambao unafanyika baada ya juhudi za vyombo vya habari nchini Kenya, unatarajiwa kufuatiliwa na mamilioni ya watu ndani na nje ya mipaka ya Kenya kupitia njia za mitandao ya kijamii pamoja na magazeti, huku vituo vinane vya televisheni, vituo 34 vya redio vikitegemewa kuutangaza moja kwa moja tukio hilo.

Kwa awamu hii ya kwanza, mdahalo huo utajikita kuangalia masuala ya uongozi, huduma za kijamii, afya na elimu pamoja na usimamizi wa rasilimali bila ya kuliacha nyuma suala la usalama.

Wagombea sita wa urais – Uhuru Kenyatta, Raila Odinga, Musalia Mudavadi, Martha Karua, Peter Kenneth na James Ole Kiyiapi – watapambana kujibu masuali na kujieleza juu ya walivyojiandaa kuyatatua matatitizo ya Wakenya katika ajenda zitakazojadiliwa.

Watangazaji watakaohusika kuwabana wagombea hao kujibu masuali yaliyoandaliwa na jopo maalum la waandalizi wa mdahalo huo ni Linus Kaikai kutoka kituo cha televisheni cha Nation na Julie Gichuru akiwa ni mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Citizen jijini Nairobi. Mdahalo huo utakaoanza saa 1:30 magharibi kwa saa za Afrika Mashariki utafanyika katika ukumbi wa shule ya kimataifa ya Brookehouse jijini humo.

Bunge la mwanzo baada ya uchaguzi wa 2007 nchini Kenya. Mdahalo huo unafanyika katika wakati ambapo tafiti za maoni zilizofanywa na mashirika mbalimbali zikionesha kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 4 Machi yatakuwa ni ya kukaribiana kabisa, hasa kati ya wagombea wakuu wawili – Raila Odinga kutoka muungano wa CORD na Uhuru Kenyatta akishikilia bendera ya muungano wa Jubilee – huku ikitajwa kuweko uwezekano mkubwa wa kufanyika duru ya pili.

Kwa mujibu wa mashirika ya kukusanya maoni ya Ipsos Synovate na Infotrack wapiga kura ambao watafuatilia kwa makini zaidi mdahalo huo ni wale ambao hadi sasa hawajaamua ni nani anayestahili kupigiwa kura kuliongoza taifa hilo kubwa kiuchumi katika eneo la Afrika Mashariki.

Wadadisi wa mambo wanasema mdahalo huo wa kwanza kabisa kuwahi kufanyika nchi humo unaweza kuwa chachu muhimu kwa wapiga kura juu ya mtu wa kumpigia kura, ingawa mtazamo utakaojitokeza baada ya mdahalo juu ya vipi matokeo ya uchaguzi yanavyoweza kuwa ni suala litakalotegemea mambo mengi.

Lakini, juu ya hilo, wakati zikiwa zimesalia wiki tatu tu kufanyika kwa uchaguzi huo mkuu na kukitarajiwa mdahalo wa pili tarehe 25 Februari, ni wazi mdahalo huo unaweza kabisa kuwashawishi wapiga kura wengi kujitokeza kuitafuta hatma ya nchi yao.

Sunday, February 10, 2013

NU JOINT: POMBE YANGU / MADEE

DJ Fetty: NU JOINT: POMBE YANGU / MADEE

AZAM YAFANYA KWELI KWA MTIBWA

AZAM FC imeikamata Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja Manungu, Turiani, Morogoro jioni hii.
Ushindi huo unaifanya Azam ifikishe pointi 33 sawa na Yanga SC, ingawa Wana Lamba Lamba wamecheza mechi moja zaidi.
Yanga inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao, kwani imefunga mabao 29, imefungwa 12 na Azam sasa imefunga mabao 27, imefungwa 14.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Azam ilitangulia kupata bao dakika ya 14, lililofungwa na beki wake Mkenya, Joackins Atudo, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Wakata Miwa..
Mtibwa, mabingwa wa Ligi Kuu mara mbili 1999 na 2000, walisawazisha bao hilo dakika ya 21, mfungaji winga wa zamani wa Yanga, Vincent Barnabas, aliyeuwahi mpira baada ya kipa wa Azam, Mwadini Ali kuteleza wakati amerudishiwa mpira na beki wake, Atudo.
Hadi mapumziko, timu hizo ziliwa zimefungana bao 1-1 na kipindi cha pili Azam walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao ya ushindi.
Azam ilipata bao lake la pili dakika moja tu tangu kuanza kipindi cha pili, 46, lililotiwa kimiani na mshambuliaji Mganda, Brian Umony aliyepokea pasi ya kiungo Mkenya, Humphrey Mieno.
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche alifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili za mwisho na kuunenepesha ushindi wa Azam.
Alifunga bao la tatu dakika ya 89, akimalizia pasi nzuri ya Mieno na la nne alifunga baada ya kupokea pasi nzuri sana ya Salum Abubakar 'Sure Boy.'
Yanga itashuka dimbani Jumatano kumenyana na vibonde, African Lyon ili kufikisha idadi ya mechi sawa na Azam na Simba SC zinazofukuzana katika mbio za ubingwa.
Simba SC waliotoa sare ya 1-1 na JKT Oljoro jana mjini Arusha, wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 28.