Mabomu yaliyolipuliwa yalisemekana kuwa ya kutengenezwa nyumbani |
Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamesema kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu madogo yaliyotengenewa nyumbani.
Mlipuko huo uliotokea muda wa asubuhi wenye shughuli nyingi,
ulisababisha kuvunjika kwa madirisha na moshi mkubwa kufuka.
Ripoti zilizotolewa na shirika la habari la kiserikali
zilisema kuwa mabomu madogo yalikuwa yamefichwa ndani ya maua kando ya
barabara.
Milipuko hiyo ilitokea Kaskazini mwa China katika eneo la,
Tai-yuan, mkoani, Shanxi,
Tai-yuan, mkoani, Shanxi,
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu
8 wamejeruhiwa na magari mawili kuharibiwa.
Picha zilizowekwa kwa mitandao ya kijamii imeonyesha moshi
ukifuka pamoja na magari ya wazima moto ikiwa katika eneo la shambulizi ambalo
lilitokea mapema asubuhi ya leo.
Hakuna taarifa za kina kueleza kiini cha milipuko hiyo. Hata
hivyo kumekuwa ma matukio ya mara kwa mara ya wananchi kufanya mashambulizi
kama haya dhidi ya serikali hasa wale ambao hawahisi kuridhishwa na serikali
hiyo.
Hali ya wasiwasi pia imetanda hasa baada ya tukio la wiki
jana mjini Beijing ambalo mamafisa walisema kuwa lilikuwa njama ya shambulizi
la kigaidi.
SOURCE; BBC
No comments:
Post a Comment