Sunday, December 30, 2012

YANGA WAKWEA PIPA KUELEKEA UTURUKI


YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wameondoka Alfajiri ya leo, saa 10:30 usiku kwenda Uturuki kuweka kambi ya mazoezi ya wiki mbili. Kikosi kizima cha Yanga kilikuwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu saa 8:00 usiku kwa taratibu za kusafiri katika ziara hiyo ya kwanza nje ya Afrika tangu walipokwenda Brazil mwaka 1974. Yanga itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia. Kikosi cha Yanga kilichoondoka Alfajiri ya leo ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani. Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza. Upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge. Mwandishi wa Gazeti la Mwanaspoti, Michael Momburi yupo kwenye ziara hiyo ya kwanza ya Yanga Ulaya, yeye akigharamiwa na kampuni yake. Ziara ya mwisho katika nchi ya maana kwa Yanga, ilikuwa mwaka 2008 nchini Afrika Kusini, ambako iliweka kambi ya zaidi ya wiki mbili wakati huo ikiwa chini ya Profesa Dusan Savo Kondic, raia wa Serbia. Zaidi ya hapo, mwaka huu Yanga ilikwenda Kigali, Rwanda kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Bara, kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Paul Kagame. Yanga SC ni klabu kongwe Tanzania ambayo kati ya zinazoshiriki Ligi Kuu kwa sasa, yenyewe ndio yenye umri mkubwa zaidi. Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini. Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba. Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani. Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza. Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini. Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao. Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana. Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs. Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam. Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga. Safari njema Yanga SC.  

AJALI YA MOTO TENA MBEYA

ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA JIJINI MBEYA KATIKA MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYABIASHARA MAARUFU WA JIJINI MBEYA (MWANJELWA).


Hayo ni mafuta yakiwa yametapaka njiani

gari ambayo imeungua vibaya na moto

baadh ya wakazi wakishangaa kilichotokea

hapo mbele ni mafuta



baadhi ya wafanya biashara wakifika eneo la tukio kuangalia kilichojili





mafuta

hiyo ni mimea ikiwa imemwagikiwa na mafuta


























Thursday, December 27, 2012



<script src="http://h1.flashvortex.com/display.php?id=2_1356609998_60992_692_0_300_250_10_1_2" type="text/javascript"></script>

Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba msaada wa Ufaransa



SERIKALI ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imevitaka vikosi vya kulinda amani vya Ufaransa kusaidia kusimamisha juhudi za waasi kuendelea kusonga mbele katika harakati zao za kuingia katika mji mkuu Bangui.
Mamia ya watu wamekusanyika jana nje ya ubalozi wa Ufaransa wakiwasilisha ombi hilo, ambalo Ufaransa haijajibu haraka lakini imesema wanajeshi zaidi wa kulinda amani wametumwa kuweka ulinzi katika ubalozi huo. Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa na Marekani wakiwataka raia wao kuondoka nchini humo.
Francois Bozize alichukua madaraka baada ya mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Ange Felix Patassé Francois Bozize alichukua madaraka baada ya mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Ange Felix Patassé
Ripoti zinasema kwamba muungano wa waasi wa Seleka umeiteka miji kadhaa katika wiki za karibuni wakati waasi hao wakisonga mble kwa kasi kuelekea mji mkuu Bangui. Muungano huo wa Seleka unasema unapambana kutekeleza mpango wa amani ili kusitisha uasi uliofanywa awali au utamwondoa rais aliyeko madarakani Francois Bozize. Umoja wa Mataifa jana Jumatano umewashutumu waasi hao kwa kusonga mbele na kuamuru zaidi ya wafanyakazi wake 200 na familia zao kuondoka nchini humo. Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Martin Nesirky ametoa taarifa inayosema Ban amelaani kabisa mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha dhidi ya miji kadhaa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kupangwa na muungano wa waasi SELEKA.
Anasema hali hii inahujumu kwa kiasi kikubwa mikataba ya amani Iliyopatikana, pamoja na juhudi za jamii ya kimataifa kutafuta amani nchini humo. Nesirky pia amethibitisha kuwa familia zote za wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wasiokuwa na majukumu makubwa zimehamishwa kutoka nchini humo. Mwakilishi maalum wa Ban, nchini humo Margaret Vogt anaendelea kuzungumza na serikali na viongozi wa waasi kwa lengo la kuhakikisha usitishwaji vita na kuanzisha mazungumzo.
Jamhuri ya Afrika ya Kati inaathirika na migogoro kutoka nchi jirani Jamhuri ya Afrika ya Kati inaathirika na migogoro kutoka nchi jirani
Hatua zilizopigwa na waasi katika wiki za karibuni ambapo wametwaa miji kadhaa zimeangazia ulegevu uliopo katika nchi hiyo, ambayo ina utajiri wa madini ya uranium na dhahabu na almasi lakini haijakuwa imara tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mnamo mwaka wa 1960.
Duru za jeshi zinasema waasi wamesonga hadi mji wa Damara, kilomita 75 kutoka mji mkuu Bangui, kufikia jana mchana, baada ya kuudhibiti mji wa Sibut ambako takribani wanajeshi 150 wa Chad awali walikuwa wamewekwa kujaribu kuwazuia waasi dhidi ya kuingia upande wa kusini.
Nchi kadhaa za Afrika ya Kati zina vikosi vyao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kama sehemu ya ujumbe wa MICOPAX, na Chad iliongeza idadi ya wanajeshi wake mapema mwezi huu. Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema badhii ya wanajeshi wakem 250 walioko nchini humo kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa MICOPAX wametumwa kuweka ulinzi katika ubalozi wao na kuwalinda raia wa Ufaransa. Marekani pia imetoa wito wa kufanywa mazungumzo wakati ikiwataka raia wake kuondoka nchini humo hadi pale hali ya usalama itakapoimarishwa. Safari ya ndege ya kila wiki ya kampuni ya Air France kutoka Paris hadi Bangui imelazimika kugeuza mkondo kutokana na hali mjini Bangui. Rais Francois Bozize aliingia madarakani mnamo mwaka wa 2003 baada ya vita vya muda mfupi na kila mara yeye hutegemea uingiliaji wa kigeni kupambana na uasi na ukosefu wa usalama nchini humo unaotokana na migogoro ya nchi jirani.

MKUU WA WILAYA MBEYA MJINI NORMAMAN SIGGALA AVUVIWA ROHO MTAKATIFU

KATIKA TAMASHA LA NYIMBO ZA INJILI LIVE LILILOFANYIKA UKUMBI WA TEKU LIKIWALIMEANDALIWA NA JP PRODUCTION PAMOJA NA HUDUMA YA JEM GOSPER MINISTRY LILODHAMINIWA NA MALAFYALE INTERTAINMENT



MKUU WA WILAYA YA MBEYA MJINI DR NORMAN SIGALLA AKILISAKATA RUMBA LIVE KATIKA TAMASHA LA CHRISTMAS LILILOFANYIKA CHUO KIKUU TEKU


JEREMIA MWAKANYILENGE AKIWA NA BANDI YAKE JP BAND WAKILISHAMBULIA JUKWAA NA KUTOA BURUDANI KWA MASHABIKI WALIOHUDHURIA TAMASHA HILO










MBEYA MORAVIANI TOWN CHOIR (KAMPUNI) WAKILIPAMBA KWA NYIMBO TAMASHA HILO NA KUKONGA MIOYO YA TAZAMAJI WALIOHUDHURIA



source=malafyale blogspot .com

Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos

Maafisa wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka LagosMoto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.

Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.Bado baadhi yamajengo yanaendelea kuteketea.Mwandishi wa BBC anasema maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.

Kwingineko, maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi kubwa ya wakristo.Msemaji wa jeshi ameiambia BBC, kuwa washambuliaji hao waliwafyetua risasi waumini katika kanisa dogo wakati wa ibada ya Krismasi.

Mshambuliaji mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.Ripoti zaidi zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini kundi lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.

Friday, December 21, 2012

Ndege ya UN yashambuliwa Sudan Kusini


UMOJA wa Mataifa umesema helicopta kutoka kwa kikosi chake cha kutunza amani Sudan Kusini imeangusha na jeshi la nchi hiyo na kuwaua watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema ndege hiyo ilishambulia wakati ilipokuwa katika harakati za kushika doria Mashariki mwa jimbo la Jonglei. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduado del Buey amesema jeshi la Sudan Kusini limekiri kushambulia helicopta hiyo. Umoja wa mataifa umekuwa ukiwasaidia raia waliokwama ndani ya mapigano kati ya jamii mbili zinazozoana katika jimbo hilo la Jonglei. ”Ripoti za mwanzo zinaashiria kuwa ndege hiyo ya Umoja wa Mataifa ilianguka na kushinda moto. Kikosi chake kilianza haraka shughuli za kutafuta mabaki na manusura wa ndege hiyo. Hata hivyo imebainika kuwa watu wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo wameuawa” msemaji huyo alisema. Lakini katika mazungumzo kati ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaotunza amani nchini Sudan Kusini na jeshi la nchi hiyo SPLA, Umoja wa Mataifa umesema wanajeshi wa Sudan Kusini wamekiri walishambulia ndege hiyo katika eneo la Likuangole katika jimbo la Jonglei. Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa chanzo cha ajali hiyo hakijulikani. Hata hivyo amekataa kuthibitisha au kukanusha kuhusika kwa wanajeshi wake.

-BBC

<script src="http://h1.flashvortex.com/display.php?id=2_1356158775_22184_692_0_300_250_10_1_124" type="text/javascript"></script>

STARS YAJIPIMA NA MABINGWA WA AFRIKA KIBOKO YA AKI...

BIN ZUBEIRSTARS YAJIPIMA NA MABINGWA WA AFRIKA KIBOKO YA AKI...: Taifa Stars Na Prince Akbar TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumeny...

BA IN SOCIOLOGY TEKU WAFANYA KIKAO

Mh. Tweve Nehemia akifungua kikao


Nzunda Enock akichangia hoja



moja ya wajumbe Chowo akiripoti kikaoni

Mwaipungu Asheri akichangia hoja



baadhi ya waliohudhuria wakitafakari kwa umakin, wa kwanza alie suka nywele ni Kayola Nanzige, katikati suti kijani Mwakalundwa Lusajo anefuata Njau Stephano




mh. Bikombo akiketi mara baada ya kuchangia hoja



wajumbe wakifuatilia mazungumzo hapo nyuma mwenye suti ya kijani ni Mwamwezi Edgar

mmoja wa waliochanngia hoja Siwingwa Josephat akiongea kwa msisitizo.



WANAFUNZI wa mwaka wa pili (BASO) katika chuo kikuu cha Teofilo kisanji university kilichopo nyanda za juu kusini mkoani Mbeya leo wamefanya kikao ili kujadili mambo mbali mbali katika chuo chao.



Akifungua kikao hicho mbunge wa BASO mwaka wa pili mh. Tweve Nehemia alianza kwa kuwapongeza wote waliofanikiwa kuhudhuria kikao hicho na hatimae kusoma ajenda mbalimbali. Tweve alizitaja ajenda hizo kuwa ni; mwenendo wa mfuko ulionzashwa na wanafunzi wa BASO ilikuwasaidia pale matatizo mbalimbali yanapo jitokeza, ushiriki wa wanafunzi katika shughuri za kitaaluma na mwisho namana ya kusaidiana katika taaluma na michango ya kufiwa na pongezi pale mmoja wao anapojifungua



Tweve aliwashukuru sana walio kabidhiwa dhamana ya kuhakikisha mfuko huo (TEKUBA) unaendelea vizuri mh. Paul Edward na Ng’ahara Zaina kwa kutekeleza jukumu lao ipasavyo.



Wakichangia ajenda ya ushirikiano katika suala la kitaalum wengi walionekana wakiwalaum baadhi ya wenzao kutoshiriki vyema katika kazi za makundi maarufu kama Group Assignment hali inayopelekea kuwapa kazi wenzao ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu, hoja iliyo changiwa na Siwingwa Josephat, Castory, Nzunda Enock, Bikombo Fidelis, Chiwambo Ausi, Ally Karafuu, Mandela Mselu, sun na kumaliziwa kwa msisitizo na Masunga Elikana.



Pia ajenda ya michango ya kufiwa na pongezi pale mmoja wao anapojifungua zilishika kasi huku ikiamriwa kuwa mchango utakuwa kwa atakaye fiwa tuu ndio utakuwa wa lazima na ule wa pongezi utakuwa hiari pale mtu mmoja mmoja atakapo jisikia na aina yoyote ya zawadi atakayo kuwa na uwezo nayo



Mwisho mbunge wa jimbo hilo Mh. Tweve aliahirisha kikao kwa kuwataka wanabaso kuwa na ushirikiano katika mambo mbali mbali hususani ya kiataaluma na kuwatakia sherehe njema za krismas na mwaka mpya kwa kuwataka wanaondoka salama na waludi salama.