Friday, November 23, 2012

YANGA YASAINI MAKUBALIANO YA UPEMBUZI AKINIFU NA BCEG




Klabu ya Yanga leo imesaini makubaliano ya upembuzi akinifu na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, juu ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa Kaunda katika eneo la makao makuu ya klabu Jangwani



Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa uongozi na kamati ya utendaji na kujadili juu ya hatua hiyo ambayo kampuni ya BCEG itaanza kazi wiki ijayo na pindi watakapokalmilisha michoro zoezi litakalofuata litakua awawu ya ujeni wenyewe.

Hiki ni kipindi cha kufanya shughuli za kimaendeleo,m na hasa kipindi hichi ambacho klabu yetu ipo katika amani namshikamano kwa viongozi na wanachama, hivyo naamin mara tutakapomaliza suala la uwanja tutaanza pia ujenzi wa jengo lakitega uchumi mtaa wa mafia alisema 'Manji'.

Naye Mkurugenzi wa shirika la BCEG nchini, bwana Geng Hijuan amesema amefurahi kufikia hatua hiyo na klabu ya Young Africans, kazi waliyopewa sasa wataifanya kwa uhakika mzuri na kutoa makadirio halisi juu ya gharama ambazo zitagharimu kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya BCEG kutoka nchini China ndiyo iliyojenga uwanja wa Taifa wa kisasa jijini Dar es salaam na sasa ndio waliopewa kazi ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Kaunda.

Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemseama, makadirio ya uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu thelathini (30,000) mpaka elfu arobaini (40,000) kutegemea na wataalam watakavyoona, pia utakua na huduma zote za muhim katika viwanja vya kisasa.

Manji alisema mategemeo ya Kamati ya Utendaji ni kuanza kujengwa kwa uwanja huo mapema kabla ya mwezi juni mwakani, ambapo desemba 8 mwaka huu watasubiria kupata baraka za wanachama katika mkutano mkuu.

No comments:

Post a Comment