Monday, October 29, 2012

PACHA WA MBUYU TWITE KABANGE TWITE AFANYA MAZOEZI NA YANGA.


Kabange Twite

Kabange $ Mbuyu Twite

Kabange Twite

Angalia picha zingine hapa chini.


Pacha wa beki wa kulipwa wa Dar es salaam Yanga Africa Mbuyu Twite anayejulikana kwa jina la Kabange Twite amekuwa akifanya mazoezi na Yanga kwa muda kama wa wiki moja sasa.

Kabange alitua Tanzania wiki iliyopita hali ambayo imepelekea kuwa na uvumi kwamba huenda akasajiliwa na klabu hiyo. Hali hiyo imepelekea kuwa na maswali mengi sana kwa wanazi na washabiki wa klabu hiyo kuwa atakayetemwa nani, kwani tayari Yanga ilishafikisha idadi ya wachezaji wa kigeni inayoruhusiwa na shirirkisho la soka Tanzania TFF.

Wachezaji hao ni Haruna Niyonzima maarufu kama fabrigas, Hamis Kiiza "Diego" Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na gorikipa Yew Berko.


Mbuyu Twite na Kabange Twite wamekuwa wanatabia ya kucheza klabu moja kwani ikumbukwe kabla ya hapo walikuwa wanakipiga na APR ya nchini Rwanda na baadae kutengana baada ya Mbyu Twite kusajiliwa na mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati.

No comments:

Post a Comment