Thursday, May 22, 2014

MANCHESTER UNITED YAMNASA TONI KROOS

 Manchester United jana usiku ilikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo Toni Kroos kutoka klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza United tayari wamekubaliana ada ya uhamisho ya £20m kwa ajili ya kiungo huyo wa Ujerumani ambaye sasa anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Bayern.
Kocha wa zamani wa United, David Moyes tayari alishamuweka Kroos kwenye mipango yake kabla ya kufukuzwa, na sasa kocha mpya wa klabu hiyo Louis van Gaal ametoa ruhusa ya kusajiliwa kwenye mchezaji huyo ambaye aliwahi kumfundisha wakati akiwa Bayern.
Baada ya miezi miwili ya mazungumzo baina ya United na Bayern, hatimaye siku chache zijazo United wanatarajiwa kumtangaza Toni Kroos kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment