Wednesday, October 31, 2012

YANGA YAIKANDAMIZA MGAMBO JKT TAIFA





Dar es salaam Yanga Africa
                            



Klabu ya Dar es salaam Yanga Africa imewaadabisha washika virungu Mgambo JKT baada ya kuwanyuka bao 3 kwa 0 bila huruma.

Yanga ambayo imeonekana kuwa na kiu kubwa ya kukalia kiti cha uongozi wa ligi kuu msimu huu mara baada ya kuanza vibaya.

Yanga imejipatia magoli yake kupiti kwa Didier Kavumbagu, Jerryson Tegete na Nadir Haroub Canavaro, huku ikiwapumulia shingoni watani wake wa jadi Simba ambao wamefungana gori 1 kwa 1 na polisi morogoro kwakuwa na pointi sawa ila Simba wakiwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.


Yanga imejipatia magoli yake kupiti kwa Didier Kavumbagu, Jerryson Tegete na Nadir Haroub Canavaro, huku ikiwapumulia shingoni watani wake wa jadi Simba ambao wamefungana gori 1 kwa 1 na polisi morogoro kwakuwa na pointi sawa ila Simba wakiwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.


Tuesday, October 30, 2012

TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU VYOMBO VYA HABARI KUZUIWA KUONESHA VPL








TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


1. Kamati ya Ligi jana (Oktoba 29,2012) ilifanya kikao pamoja na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kujadili mambo kadhaa, likiwemo tukio la Jumamosi iliyopita la kuzuia televisheni na radio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu pamoja na wapiga picha za televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari. Kamati ilifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Juma Pinto kuhusu msukosuko huo na kufikia muafaka katika masuala yafuatayo:

 a- kwamba uamuzi wa kuzuia vituo vya redio na televisheni kutangaza moja kwa moja ulikuwa sahihi lakini una kasoro katika utekelezaji kwa kuwa hayakuwepo mawasiliano rasmi kwa vyombo vya habari na pia haukutoa muda wa kutosha kwa vyombo hivyo vya habari kufanya maandalizi kwa kadri ya utashi wa klabu za Ligi Kuu.



b- Kwamba Kamati ya Ligi haijakataza redio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu, bali vituo vya redio ambavyo vinataka kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu vifanye hivyo bila ya kuweka matangazo ya wadhamini na kama matangazo hayo ya moja kwa moja yatadhaminiwa, basi vituo hivyo havina budi kuwasiliana kwa maandishi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa maelekezo zaidi.



c- Kwamba vituo vya redio vitakavyotaka kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu, ni lazima zitamke mashindano hayo kuwa ni “Ligi Kuu ya Vodacom”.



d- Kwamba vituo vya televisheni vitakavyotaka kutangaza moja kwa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, ni lazima viingie mkataba na TFF ambao utaaridhiwa na klabu husika. Kwa sasa, kituo cha televisheni cha Star TV hakitaruhusiwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya michezo hiyo hadi hapo mkataba utakaposainiwa na tunatumaini mkataba huo utasainiwa kabla ya mechi za kesho na hivyo kuwapa fursa wapenzi wa soka wa maeneo mbalimbali kuendelea kushuhudia Ligi Kuu ya Vodacom.



e- Kwamba vituo vya televisheni vitakavyotaka kuchukua picha kwa ajili ya habari zinaruhusiwa kufanya hivyo. Endapo kituo hicho kitaonesha mchezo uliorekodiwa, hatua zitachukuliwa dhidi ya kituo hicho.



f- Kamati inaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na uamuzi huo, lakini inazidi kusisitiza kuwa uamuzi huo ulifanywa kwa lengo zuri la kuendelea kutafuta vyanzo vya fedha vitakavyoziwezesha klabu kujimudu kiuchumi na kuifanya Ligi Kuu ya Vodacom iendeshwe kwa ubora zaidi.



2. Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Kim Poulsen amerejea Dar es salaam baada ya kufanya ziara kwenye visiwa vya Pemba na Unguja ambako alishuhudia mechi sita za Ligi Kuu ya Grand Malta kuanzia Oktoba 19, 2012 hadi Oktoba 26, 2012 visiwani Zanzibar. Poulsen alishuhudia mechi baina ya Falcom na Bandari iliyoisha kwa Falcom kushinda kwa mabao 3-1 na pia mechi baina ya Duma na Bandari ambayo iliisha kwa Bandari kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mechi hizo mbili zilifanyika kisiwani Pemba.



Poulsen pia alishuhudia mechi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja ambako Mtendeni iliibwaga Chipukizi kwa mabao 2-1; Mundu na Jamhuri (0-1), KMKM na Zimani Moto (1-0); na Mafunzo dhidi ya Chuoni iliyoisha kwa Mafunzo kulala kwa mabao 3-0.



Poulsen amefurahishwa na ziara hiyo na kusema kuwa ni kitu kizuri kwake na kwa soka la Tanzania kwa ujumla. Poulsen alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyopata visiwani Zanzibar na kukishukuru Chama cha Mpira wa Miguu cha Zanzibar (ZFA) kwa ushirikiano mkubwa alioupata wakati wote akiwa Zanzibar.



Hata hivyo, Poulsen alisema hawezi kueleza kwa sasa kama ameona wachezaji anaoweza kuwaita kwenye kikosi cha Taifa Stars, lakini akasema amevutiwa na viwango vya wachezaji wengi.



3. TFF inapenda tena kuihimiza klabu ya Yanga kumalizana na mchezaji wake wa zamani, John Njoroge Mwangi kabla ya Novemba 2, 2012 ili ijiepushe na adhabu kaili inayoweza kuchukuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa barua ya FIFA, iwapo Yanga haitakuwa imemlipa mchezaji huyo na kusiwepo na mawasiliano yoyote, shauri hilo litawasilishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya FIFA itakayokutana Novemba 14, 2012 kutathmini hukumu iliyotolewa mapema Januari mwaka huu.



4. Mchezo namba 10 wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baina ya Morani na Polisi Tabora uliokuwa uchezwe Kiteto mjini Tabora Oktoba 31, 2012, sasa utachezwa Novemba 01, 2012 baada ya treni ambayo Morani walikuwa wakisafiria kutoka kupata matatizo njiani wakati wakitoka Kigoma ambako walicheza na Kanembo.



5. TFF inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari leo, likiwemo gazeti la Habari Leo na Daily News, vikimnukuu rais wa TFF, Leodegar Tenga akisema kuwa amewataka watu wanaotaka kugombea uongozi wa shirikisho watangaze nia ili wapate kujadiliwa. Waandishi walioandika habari hiyo hawakumnukuu vizuri Rais Tenga wakati akizungumzia masuala ya uchaguzi na hivyo kupotosha maana nzima ambayo Ndg. Tenga alitaka iwafikie wapenzi wa michezo na hasa mpira wa miguu. Rais Tenga alivitaka vyombo vya habari vianzishe mjadala utakaowashirikisha wapenzi wa mpira wa miguu ili waelezee wanatarajia nini katika miaka ijayo na hivyo kuwafanya viongozi watakaochaguliwa kufanya kazi kwa utashi wa maoni hayo ya wananchi. Tunaelewa kuwa Rais Tenga ni muumini wa kuheshimu katiba, sheria na kanuni na hivyo hawezi kutoa kauli ambayo inakiuka mchakato wa uchaguzi wa TFF kwa kuwataka wanaowania uongozi kutangaza nia sasa badala ya kusubiri muda wa kikanuni ufike. Ikumbukwe katika kikao chake na wahariri aliwahi kuulizwa swali kama hilo na akasema kuwa akijibu lolote atakuwa amekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwa itamaanisha anaanza kampeniu kabla ya muda. Ni vizuri waliohusika wakafanya masahihisho ili kuzuia habari zao kutafsiriwa tofauti na wadau wa mpira wa miguu na hivyo kuweka uwezekano wa kuvuruga mchakato wa uchaguzi.



6. TFF imebadilisha tarehe ya kuanza kuchukua fomu kwa watu wanaotaka kugombea uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Dar es salaam (DRFA) kwa lengo la kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa kanuni. Kamati ya Uchaguzi ya DRFA ilitangaza jana kuwa uchukuaji fomu ungeanza leo, lakini DRFA iliandikiwa barua jana kuelezwa kuwa mchakato huo sasa utaanza kesho na uchaguzi utafanyika Desemba 12, 2012.



Mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa DRFA utakuwa kama ifuatavyo:

 30/10/2012 Kamati ya Uchaguzi DRFA kutangaza uchaguzi na nafasi

 Zinazogombewa kwa mujibu wa katiba ya DRFA

 31/10/2012 Kuanza kuchukua fomu za kugombea uongozi

 04/11/2012 Mwisho wa kurudisha fomu ifikapo saa 10:00 alasiri

 05-09/11/2012 Kamati ya Uchaguzi DRFA kupitia fomu za waombaji uongozi na

 kutangaza matokeo na kubandika kwenye mbao majina ya waombaji uongozi.

 10-14/11/2012 Kutoa fursa ya pingamizi dhidi ya waombaji uongozi. Pingamizi

 ziwasilishwe kwa katibu wa Kamati ya Uchaguzi DRFA na

 wawekaji pingamizi wazingatie Ibara ya 11 (2) ya Kanuni za

 Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

 15-17/11/2012 Kujadili pingamizi, usaili na kutangaza matokeo ya usaili na

 kuwajulisha kwa maandishi.

 18-20/11/2012 Kukataa rufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA



21-25/11/2012 Rufaa kusikilizwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kutangaza

 matokeo ya rufaa (Kama hakuna rufaa, Kamati ya Uchaguzi ya

 DRFA kutangaza majina ya wagombea na nafasi wanazogombea

 na kuanza kampeni).

 26/11/2012 Baada ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya

 Uchaguzi ya DRFA kutangaza majina ya wagombea na nafasi zao

 na kuanza kwa kampeni



12/12/2012 Uchaguzi

AZAM YAAMUA KUMRUDISHA STEWART HALL BAADA YA JANA KUMTIMUA BUNJAK

MoroNew: AZAM YAAMUA KUMRUDISHA STEWART HALL BAADA YA JANA KUMTIMUA BUNJAK

MH. BENARD MEMBE ATEMBELEA MPAKA WA TZ NA MALAWI NA KUONGEA NA WAZEE KYELA(MBY)




waziri Membe akiaangalia mpaka wa Tz  na  Malawi

kamati ya ulinzi na usalama wakimsikiliza waziri


mkuu wa wilaya ya kyela Mhe. M. Malenga

Waziri na kamati yake mpakani


mkuu wa wilaya ya Kyela akimuongoza waziri kuelekea mpakani

ziwa nyasa

waziri Membe

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mzozo kuhusiana na mpaka kati ya tanzania na malawi hali ambyo imelekea sintofahamu miongoni mwa watanzania waliowengi hususani wale wanaoishi mpakani.


Kufuatia hali hiyo waziri wa mambo ya nje na ushirikiaona wa kimataifa wa tanzania mh. Benard Membe amefanya ziara mkoani Mbeya na kuenda moja kwa moja wilani kyela na kwenda kujionea kinachoendelea huko.

Membe alifanikiwa kuongea na wazee wakazi wa huko mpakani ambapo alianza kwa kuwatoa hofu wazee hao kwa kuwaambia kuwa wasiwe n wasiwasi watakuwa salama na waendelee kutumia maji ya ziwa nyasa kwani ni halali yao na ni rasilimali waliyopewa na mwenyezi mungu wala hakuna mtu alichimba ziwa hilo.

Membe alianza kwa kutoa historia fupi anayoifahamu kuhusiana na mpaka huo, na baadae wazee mbalimbali wakazi wa hapo walipata fursa ya kutoa historia wanayoifahamu.




Wakiongea kwa nyakati tofauti wazee hao waliweza kutoa historia mbalimbali kuhusu mpaka huo na kutoa mambo mengine ambayo hata Mh. Membe alibaki kushangaa kwani hajawahi kusikia, hali ambayo ilimpelekea waziri kuwasikiliza kwa umakini.

"Hao wameshindwa ya kuongea kuhusiana na mpaka huu kwani hata hivi kuna makaburi ya babu na bibi zetu yamekwisha mezwa na ziwa, kuanzia hapa tulipo ni km kazaa kwenda mbele ndipo mpaka ulikuwa kipindi cha utawala wa Mjerumani na kithibitisho ni kwamba yule Mjerumani kuna mibuyu ipo kule iligongwa mihuri miwili isiyofutika ikisomemeka Tanganyika territory paka leo ipo.

Akaendelea kwa kusema kuna kitabu kilichotolewa kipindi cha Mjerumani wa kwanza ambaye alikuja kuleta dini ya Moravian ukurasa wa 13 kinaelezea vizuri kuhusu mpaka huu, akatoa kitabu". Mzee

Hata hivyo waziri kwa heshima na taadhima alimumba huyo mzee hicho kitabu kama ushahidi na akaahidi kukirudisha mara baada ya kukifanyia kazi.

Akihitimisha waziri aliwashukuru wote waliohusika na kuwataka kuwa na amani na kuendelea na shughuli za kiuchumi kama kawaida.

"Tutaenda Ujerumani, Uingereza na Addis Ababa nchini Ethiopia yaliko makao makuu ya umoja wa kimataifa ilikupata vielelezo vya kutosha" alisema Membe.




Monday, October 29, 2012

Boris Bunjak atupiwa virago Azam FC





Klabu ya Azam FC imeamua kumtupia virago kocha wake mserbia Boris Bunjak.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom zinasema kwamba kocha huyo ametimuliwa rasmi kukinoa kikosi hicho cha wanalambalamba.

Ikumbukwe kuwa mserbia huyo alisaini mkataba wa miaka 2 kuifundisha klabu hiyo, mara baada ya kocha Stewart Hall kutimuliwa.

Habari kutoka ndani ya klabu hoyo zinasema viongozi wapo katika mchakato wa kumrudisha kocha wao wa zamani muingereza Stewart Hall  ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Sofa paka ya Kenya.

Hatua ya kumtupia virago kocha Boris Bunjak imekuja mara baada ya Azam FC kuambulia kichapo cha 3 – 0 kutoka kwa vinara wa ligi kuu Simba Sports Club.

PACHA WA MBUYU TWITE KABANGE TWITE AFANYA MAZOEZI NA YANGA.


Kabange Twite

Kabange $ Mbuyu Twite

Kabange Twite

Angalia picha zingine hapa chini.


Pacha wa beki wa kulipwa wa Dar es salaam Yanga Africa Mbuyu Twite anayejulikana kwa jina la Kabange Twite amekuwa akifanya mazoezi na Yanga kwa muda kama wa wiki moja sasa.

Kabange alitua Tanzania wiki iliyopita hali ambayo imepelekea kuwa na uvumi kwamba huenda akasajiliwa na klabu hiyo. Hali hiyo imepelekea kuwa na maswali mengi sana kwa wanazi na washabiki wa klabu hiyo kuwa atakayetemwa nani, kwani tayari Yanga ilishafikisha idadi ya wachezaji wa kigeni inayoruhusiwa na shirirkisho la soka Tanzania TFF.

Wachezaji hao ni Haruna Niyonzima maarufu kama fabrigas, Hamis Kiiza "Diego" Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na gorikipa Yew Berko.


Mbuyu Twite na Kabange Twite wamekuwa wanatabia ya kucheza klabu moja kwani ikumbukwe kabla ya hapo walikuwa wanakipiga na APR ya nchini Rwanda na baadae kutengana baada ya Mbyu Twite kusajiliwa na mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati.

BAADA YA DEAR GOD KUFANYA POA KALA ASEMA KUWA ANAF...

BAADA YA DEAR GOD KUFANYA POA KALA ASEMA KUWA ANAF...: Msanii anayefanya poa hivi sasa na ngoma ya 'Dear God' amesema kuwa toka atoe wimbo wake wa 'Dear God' amepata maombi mengi kutoka kwa wa...

Sunday, October 28, 2012

CHAMA CHA MPIRA MKOANI MBEYA CHAPATA VIONGOZI WAPYA.



CHAMA cha mpira wa miguu mkoani Mbeya ( MREFA) kimepata viongozi wake katika uchaguzi  uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lungwe.

Akiongea na Hottest Newz katibu wa kamati ya uchaguzi huo Prince Mwaihojo aliwatataja walioibuka kidedea katika uchaguzi huo kuwa ni nafasi ya (Mwenyekiti)  John David Mwamwaja, (Makamu mwenyekiti) ni Omary Daud  Mkwawa Mahinya, nafasi ya (katibu) ni Seleman Haroub Said, (katibu msaidizi) ni William Wilson Mwamlima.

Mwaihojo aliwataja wengine kuwa ni wajumbe mwakilishi Taifa Oscar Donald Korosso, (mjumbe Mwakilishi vilabu) ni Juma Beblon Killa na nafasi ya (Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji) ni Dickson Lusubilo Sinkwembe, Andongwisye Ramadhan Panja na Lwitiko Edward Mwamndela.

Aidha Mwaihojo aliwashukuru wote waliofanikisha uchaguzi huo kufanyika kwa amani na kuwapongeza wote walioshinda uchaguzi huo.

Naye mwenyekiti mpya wa (MREFA) John David Mwamwaja amewataka viongozi wenzake walioshinda uchaguzi na wale walioshindwa katika kinyang’anyiro hicho kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha maendeleo ya soka katika mkoa wa Mbeya.




Thursday, October 25, 2012

Wema Sepetu & Diomond (LIVE Perfomance @Fiesta Morogoro)

shooting mpya DEAR GOD-KALA JEREMIAH

KASSIM-HAIWEZEKANI- By Cassim kati ya video ninazozikubali.

PICHA ZA MAMBO YALIVYOKUWA YANGA AKAWADUNGUA POLSI...

PICHA ZA MAMBO YALIVYOKUWA YANGA AKAWADUNGUA POLSI...:   Mchezaji wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam David Luhende akimiliki mpira mbele ya Nicholas Kabipe beki wa timu ya polisi ...

BREAKING NEWS! KIKOSI CHA PRISONS FC CHAPATA AJALI...

 BREAKING NEWS! KIKOSI CHA PRISONS FC CHAPATA AJALI...: Timu ya prison ya Mbeya imepata ajali eneo la Hare mkoani Tanga,wachezaji Issa Mwantika,Lugano Mwangama,Khalidi Fungabreki,Daudi Masungwe wa...

MASKINI SHILOLE!UDAKU KUTOKA GLOBAL PUBLISHER, AN...

UJANATZ: 'MASKINI SHILOLE!UDAKU KUTOKA GLOBAL PUBLISHER, AN...: Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa ameanika sehemu zake za siri. Gazeti hili lina picha zinazomwonesha Shilole ambaye kwa sasa amegeukia mu...

Tuesday, October 23, 2012

From AnnaPeter

AnnaPeter: KAMANDA WA POLISI CHARLS KENYELA AZUNGUMZIA TUKIO ...: Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Bwana Charles Kenyela Kamanda wa Polisi Charles Kenyela pichani amezungumzia kuhusu tukio ...

Monday, October 22, 2012

Godfrey Bonny Mwandanje arudi kuiongezea Mbeya City nguvu.




TIMU ya soka ya Mbeya City ya jijini Mbeya inayoshiriki ligi daraja la kwanza Taifa imetamba kufanya vizuri katika mashindano hayo na kupanda daraja ili kucheza ligi kuu Tanzania bara katika msimu ujao.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalwis aliiambia Hottest newz kuwa mwaka huu hawatakubali tena kukosa nafasi ya kucheza mashindano ya Ligi kuu mwakani kutokana na jinsi walivyo jipanga.

Alisema maandalizi yao yako vizuri na wako tayari  kupigana mpaka dakika ya mwisho ili waweze kufuzu fainali na kufanikiwa kuwa miongoni mwa timu zitakazo panda daraja msimu huu.

Mwalis alisema ili kufanikisha lengo lao la kupanda daraja wameawasajili baadhi ya wachezaji wazoefu akiwamo Godfrey Bonny Mwandanje ambao watawasaidia katika harakati za kufanya vizuri.

“Tumejipanga sana hatutafanya makosa kama msimu uliopita , tumerekebisha makosa mbalimbali yaliyotufanya tukashindwa kupanda daraja licha ya kuwa tulianza vizuri lakini msimu huu tutaanza kwa kasi na kumaliza vizuri” alisema Mwalis.

Alisema licha ya timu nyingi kujiaandaa sana na ugumu wenyewe wa ligi daraja la kwanza, lakini kikosi chao kimepata muda mwingi wa kujiandaa na kufanya marekebisho yaliyo jitokeza msimu ulio pita.

Aidha Mwalwis alisema kuwa timu yake imepangwa katika kundi A, pamoja na timu za Majimaji ya Songea, Bukinafaso ya Morogoro , Kurugenzi ya Mufindi, Small kids ya Sumbawanga, Mlale ya Ruvuma, Polis ya Iringa na Mkamba ya Morogoro.

Ligi hiyo ya daraja la kwanza inatarajia kuanza juma tano  ambapo Mbeya City itakuwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakikaribishwa na wenyeji Bukina Faso ya mjini hapo.







Sunday, October 21, 2012

Ratiba Ligi Daraja la Kwanza goup A. Mbeya city, Kurugenzi na Polisi Iringa ndani.


TANZANIA FOOTBALL FEDERATION.


1st DIVISION LEAGUE – GROUP “A” 2012/2013 – FIRST ROUND

DATE                                         TEAMS                                     VENUE

24Oct. 2012               BURKINAFASO Vs MBEYA CITY       JAMHURI MOROGORO
                                  MLALE Vs SMALL KIDS--------------- MAJIMAJI RUVUMA
                                  KURUGENZI Vs MAJIMAJI-----------WAMBI MUFINDI-IRNG
                                  MKAMBA Vs POLISI IRINGA--------JAMHURI MOROGORO

27Oct. 2012              POLISI IRINGA Vs MBEYA CITY-----SAMORA IRINGA
                                 MAJIMAJI Vs SMALL KIDS-------------MAJIMAJI RUVUMA
                                 BURKINAFASO Vs MKAMBA----------JAMHURI MOROGORO
                                 KURUGENZI Vs MLALE-----------------WAMBI MUFINDI IRNG

31Oct. 2012               MBEYA CITY Vs MLALE----------------SOKOINE MBEYA
                                  SMALL KIDS Vs MKAMBA -------------MANDELA RUKWA
                                  MAJIMAJI Vs BURKINAFASO----------- MAJIMAJI RUVUMA
                                  POLISI IRINGA Vs KURUGENZI -------- SAMORA IRINGA

4Nov. 2012                SMALL KIDS Vs MBEYA CITY ----------- MANDELA RUKWA
                                  MLALE Vs MKAMBA ----------------------- MAJIMAJI RUVUMA
                                  KURUGENZI Vs BURKINAFASO -------- WAMBI MUFINDI
                                  POLISI IRINGA Vs MAJIMAJI------------- SAMORA IRINGA

7Nov.2012                MBEYA CITY Vs KURUGENZI------------ SOKOINE MBEYA
                                  BURKINAFASO Vs SMALL KIDS --------JAMHURI MORO
                                   MLALE Vs POLISI IRINGA ---------------- MAJIMAJI RUVUMA

8 Nov. 2012              MKAMBA Vs MAJIMAJI ------------------- JAMHURI MORO
                                
11 Nov. 2012            MAJIMAJI Vs MLALE ----------------------  MAJIMAJI RUVUMA
                                  MKAMBA Vs MBEYA CITY -------------- JAMHURI MORO
                                  KURUGENZI Vs SMALL KIDS -----------WAMBI MUFINDI
                                  POLISI IRINGA Vs BURKINAFASO ----- SAMORA IRINGA

14 Nov.2012             SMALL KIDS Vs POLISI IRINGA --------- MANDELA RUKWA
                                  MBEYA CITY Vs MAJIMAJI --------------- SOKOINE MBEYA
                                  MKAMBA Vs KURUGENZI ----------------- JAMHURI MORO
                                  MLALE Vs BURKINAFASO -----------------MAJIMAJI RUVUMA

                                                  

Ingoma inogile sokoine, wajelajela waua.



Kocha wa Tanzania Prisons Jumanne Chale akiwaongoza vijana wake kwenda  kwenye vyumba vya kubadilishia nguo

Tanzania p wakifanya warm up kujiandaa kuingia uwanjani.

Toto African wakinyosha misuli kujiandaa kuingia uwanjani.

Lugano Mwangama jezi nyeupe nahodha wa tz p. na nahodha wa  Toto African wakiwa na waamuzi .

Mchezo ulimalizika kwa wajelajela tanzania Prisons kuwatandika Toto African gori 1 - 0. Gori hilo lilipatikana kunako dakika ya 33 ya mchezo kupitia kwa kiungo wao machachali Peter Michael akiunganisha kona safi iliyochongwa na Henry mwalugala kutoka magharibi mwa uwanja.

Baaada ya hapo vijana wa Tanzania Prisons waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao kama nyuki huku wakiwatumia washambuliaji wao wa pembeni Augustino Tino, John Matei na Misango Magai.

Kipndi cha pili kilianza kwa Toto African kuzinduka na kufika mara kadhaa langoni mwa wapinzani wao kupitia kwa washambuliaji wao Emaanuel Swita, Seleman Kiputa na Kheri Mohamed, lakini uimara wa kipa na safu yote ya ulinzi ya Prison ilikuwa kikwazo kwao kupata gori la kusawazisha kwani mpaka mwamuzi Simon Mbelwa kutoka pwani anapuliza kipenga chake cha mwisho matokeo haya kubadilika.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa timu ya Tanzania Prisons katika uwanja wake wa nyumbani, na kwa ushindi huo Tanzania  Prisons imekwea mpaka nafasi ya sita kwa kujikusanyia jumla ya pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara 9. Uhindi huo umepokelewa kwa shangwe kubwa na wadau pamoja na mashsbiki wa soka Jijini Mbeya.

Katika viwanja vingine mzimu wa sare umeendelea kuiandama timu ya Simba baada ya kutoshana nguvu na Mgambo Jkt huko Mkwakwani, Jkt Oljolo 1-1 na  Jkt Ruvu katika uwanja wa chamazi.



MTAZAMO: RATIBA YA LIGI DARAJA LA KWANZA

MTAZAMO: RATIBA YA LIGI DARAJA LA KWANZA: TANZANIA FOOTBALL FEDERATION Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA ...

Saturday, October 20, 2012

Shaffih Dauda in Sports.: NDOTO YA MBWANA SAMATA NA ULIMWENGU KUCHEZA FAINAL...

Shaffih Dauda in Sports.: NDOTO YA MBWANA SAMATA NA ULIMWENGU KUCHEZA FAINAL...

VPL kuendelea kutimua vumbi hapo kesho, Toto African Vs Tz Prisons.


Add caption







VPL kuendelea kutimua vumbi hapo kesho, Toto African Vs Tz Prisons.


Add caption







VPL kuendelea kutimua vumbi hapo kesho, Toto African Vs Tz Prisons.

Wachezaji wa Timu ya Toto African wakimsikiliza kocha wao kujiaandaa na mpambano hapo kesho


John Tegete akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.



Toto African wakifanya mazoezi ya mwisho kujiandaa kukabiliana na maafande wa Tanzania Prisons.

mlinda mlango wa Toto African

Kikosi cha maafande wa  Tanzania Prisons watakaoshuka dimba hapo kesho kusaka pointi tatu mhimu katika dimba lao la nyumbani Sokoine. 

AnnaPeter: BAADA YA BELE 9 KUTOKA HIKI NDO KIPAJI KINGINE KIL...

AnnaPeter: BAADA YA BELE 9 KUTOKA HIKI NDO KIPAJI KINGINE KIL...: Anaenda kwa jina la Bright ni msanii mpya ambaye hivi sasa kazi zake zinasimamiwa na Monagengsta,ni kipaji kipya ambacho produza huyo ana...

AnnaPeter: BAADA YA BELE 9 KUTOKA HIKI NDO KIPAJI KINGINE KIL...

AnnaPeter: BAADA YA BELE 9 KUTOKA HIKI NDO KIPAJI KINGINE KIL...: Anaenda kwa jina la Bright ni msanii mpya ambaye hivi sasa kazi zake zinasimamiwa na Monagengsta,ni kipaji kipya ambacho produza huyo ana...

MoroNew: VODACOM WAWATENGENEZEA YANGA NEMBO YAO PEKE YAO

MoroNew: VODACOM WAWATENGENEZEA YANGA NEMBO YAO PEKE YAO: Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya...

MoroNew: LIGI KUU TANZANIA BARA LEO: YANGA YAIPIGA RUVU S...

MoroNew: LIGI KUU TANZANIA BARA LEO: YANGA YAIPIGA RUVU S...:  Mabingwa wa KAGAME leo wameinyuka timu ya  Ruvu Shooting  magoli 3-2 katika mchezo mkali na wakusisimua uliopigwa uwanja wa Taifa Ruvu...

Friday, October 19, 2012

Makambako Kwetu: BREAKING NEWS: Kariakoo hali si shwari

Makambako Kwetu: BREAKING NEWS: Kariakoo hali si shwari: Polisi walazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa dini ya kiislam wanaoleta fujo eneo la Kariakoo. Kwa habari zaidi fu...

Meneja wa uwanja wa Sokoine akanusha kufungiwa kwa uwanja

uwanja wa sokoine mbeya.






MENEJA Modestus Mwaluka wa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambao unatumiwa  na timu ya Tanzania Prisons kama Uwanja wa nyumbani amekanusha taarifa ya vyombo vya habari kuwa upo hatarini kufungiwa na TFF  kutokana na ubovu.
                           
Uwanja wa huo hivi karibuni umekuwa ukilalamikiwa na baadhi ya timu ambazo hushuka katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara kuwa pichi yake ni mbaya na haufai kutumika kwa mashindano ya ligi.

Akizungumza na Hottest newz jana Mwaluka alikanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya habari nchini kuwa uwanja huo upo hatarini kufungiwa na Shirikisho linalo simamia mpira wa miguu TFF.

“Hatujapata taarifa zozote kutoka TFF za kuhusu kufungiwa uwanja wetu, zaidi ya kuambiwa turekebishe wigo wa pembeni mwa  uwanja baada ya mchezo kati ya Prisons naYanga, ambao tayari turisha rekebisha haraka baada taarifa hiyo.” Alisema Mwaluka.

Mwaluka alisema kuwa malalamiko mbalimbali wanayopata kutoka  timu zinazoshiriki ligi kuu ni changamoto kwao na wanaendelea kuyafanyia kazi ili kuuweka sawa uwanja huo.

Mwaluka pia alisema huduma za vyoo uwanjani hapo kuwa ni nzuri na vipo vya   kutosha tofauti na vyombo vya habari vilivyo ripoti hivi karibuni.

“Vyoo vipo 6 ambavyo vinakizi kabisa  huduma kwa mashabaki wote wanaongia uwanjani, “ alisema Mwaluka.

Aidha Mwaluka alisema kuwa uwanja huo wa Sokoine unaonekana kukosa sifa ni kutokana na malekebisho makubwa waliyoyafanya msimu huu ya kuondoa vinundu uwanjani vilivyo kuwa vinapoteza umilikaji wa mpira kwa wachezaji.

“Tulikwetua uwanja kwa lengo la kutoa vinundu vilivyo kuwa vinasumbua wachezaji lakini baada ya kumaliza kukwetua kumejitokeza vishimo vidogovidogo ambavyo tunaendelea marekebisho wakati ligi inaendelea,”alisema Mwaluka.

“Kufikia mzunguko wa pili wa ligi kuu pichi ya uwanja itakuwa imekamilika vizuri kuliko ilivyokuwa mwanzo kabla ya marekebisho na malalamiko hayatajitokeza tena.” alisema Mwaluka.

Wakati huo naye mmoja wa watu wanao husika na usafi uwanjani hapo Elizabeth Mwakyoma aliwataka mashabiki  wanao hudhuria uwanjani kwa ajili ya kuangalia mpira kutumia vizur huduma ya vyoo ili kuepusha hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa, na kuwarahisishia ufanyaji wa usafi baada ya mchezo.







Wednesday, October 17, 2012

Tanzania Prisons Vs Azam FC hakuna mbabe leo Sokoine.

hapo juu ni kikosi cha wanalambalamba Azam FC kabla ya mechi

Tanzania Prisons maarufu kama wajelajela kabla ya mechi

Azam FC wakipga dua.

benchi la Azam FC









Tanzania Prisons
Mara baada ya mpambano huo kumalizika hottest newz imebahatika kuongea na walimu wa pande zote mbili ikianzia na kocha msaidizi wa Azam Kalimangonga Ongara ambaye moja kwa moja lawama zake amewatupia waamzi, kwamba hawajaitendea haki timu yake.

Kwa upande wa wanajelajela kocha wao Jumanne Charle alidhidi kusisitiza kuwa kikosi chake kimekuwa kikiimalika kila kukicha ila akaendelea kwa kusema timu yake imekuwa haifanyi vizuri kwenye safu ya ushambuliaji na kuahidi kuawapa mbinu zaidi vijana wake wanaocheza kwenye nafasi hiyo

Tanzania Prisons wametandaza kandanda safi la kuvutia katika mechi hiyo kiasi ambacho imewafanya watu wengi waliohudhuria mechi hiyo kuishangila kwa nguvu tofauti na mechi zilizopita.