TIMU ya soka ya Mbeya
City ya jijini Mbeya inayoshiriki ligi
daraja la kwanza Taifa imetamba kufanya vizuri katika mashindano hayo na
kupanda daraja ili kucheza ligi kuu Tanzania bara katika msimu ujao.
Kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalwis aliiambia Hottest newz kuwa mwaka huu hawatakubali
tena kukosa nafasi ya kucheza mashindano ya Ligi kuu mwakani kutokana na jinsi
walivyo jipanga.
Alisema maandalizi yao
yako vizuri na wako tayari kupigana
mpaka dakika ya mwisho ili waweze kufuzu fainali na kufanikiwa kuwa miongoni
mwa timu zitakazo panda daraja msimu huu.
Mwalis alisema ili kufanikisha lengo lao la kupanda daraja
wameawasajili baadhi ya wachezaji wazoefu akiwamo Godfrey Bonny Mwandanje ambao
watawasaidia katika harakati za kufanya vizuri.
“Tumejipanga sana hatutafanya
makosa kama msimu uliopita , tumerekebisha
makosa mbalimbali yaliyotufanya tukashindwa kupanda daraja licha ya kuwa
tulianza vizuri lakini msimu huu tutaanza kwa kasi na kumaliza vizuri” alisema
Mwalis.
Alisema licha ya timu nyingi kujiaandaa sana na ugumu wenyewe wa ligi daraja la
kwanza, lakini kikosi chao kimepata muda mwingi wa kujiandaa na kufanya
marekebisho yaliyo jitokeza msimu ulio pita.
Aidha Mwalwis alisema kuwa timu yake imepangwa katika kundi
A, pamoja na timu za Majimaji ya Songea, Bukinafaso ya Morogoro , Kurugenzi ya
Mufindi, Small kids ya Sumbawanga, Mlale ya Ruvuma ,
Polis ya Iringa na Mkamba ya Morogoro.
Ligi hiyo ya daraja la kwanza inatarajia kuanza juma
tano ambapo Mbeya City
itakuwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakikaribishwa na wenyeji
Bukina Faso ya mjini hapo.
No comments:
Post a Comment