Hiki ni kikosi cha maafande wa Jkt Oljoro |
wachezaji wa Tanzania Prisons |
nahodha wa Tanzania Prisons na wa Jkt Oljoro wakipeana mikono na waamzi |
Na haya ni baadhi ya matukio ya uwanjani kwa upande wa watazamaji |
Wimbi la kutofanya vizuri kwa
Wajelajela Tanzania
Prisons limeendelea kuiandama katika uwanja wao wa nyumbani Sokoine ni baada ya
jana kuangukia pua dhidi ya Maafande wenzao wa JKT Oljoro kwa jumla ya goli
1-0,
Katika pambano hilo
iliwachukua dakika tano Oljoro kuandika goli lililofungwa kiufundi na Amir Omar
baada ya kuunganisha kros safi iliyopigwa kutoka
winga ya kulia na kumkuta mfungaji wa goli hilo pekee.
Katika pambano hilo Prisons itabidi ijilaamu yenyewe kwa
kukosa magol mengi ya wazi katika dakika za 15, 34, 38, 60 na 85 kupitia kwa
washambuliaji wake.
Baada ya mechi hiyo Kocha Mkuu wa
Prisons Jumanne Charlse alitoa lawama kwa washambuliaji wake kwa kukosa umakini
uliosababisha kukosa mgoli mengi ya wazi,
Kwa upande mwingine mashabiki wa
soka jijini Mbeya walikasirishwa sana na
mwenendo wa timu yao
katika mechi zinazofanyika katika uwanja wao wa nyumbani.
Pamoja na kipigo hicho Tanzania Prisons jumatano ya wiki hii watakuwa
na kibarua kingine kigumu dhidi ya timu ngumu ya Azam FC ,maarufu kama
Wanalambalamba kutoka Dar es Salaam
ambao wanashikilia nafas ya pili katika mwendelezo wa ligi kuu .
No comments:
Post a Comment