uwanja wa sokoine mbeya.
MENEJA Modestus Mwaluka wa uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya ambao unatumiwa
na timu ya Tanzania
Prisons kama Uwanja wa nyumbani amekanusha taarifa
ya vyombo vya habari kuwa upo hatarini kufungiwa na TFF kutokana na ubovu.
Uwanja wa huo hivi karibuni umekuwa
ukilalamikiwa na baadhi ya timu ambazo hushuka katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara
kuwa pichi yake ni mbaya na haufai kutumika kwa mashindano ya ligi.
Akizungumza na Hottest newz
jana Mwaluka alikanusha taarifa iliyotolewa na baadhi
ya Vyombo vya habari nchini kuwa uwanja huo upo hatarini kufungiwa na
Shirikisho linalo simamia mpira wa miguu TFF.
“Hatujapata taarifa zozote kutoka
TFF za kuhusu kufungiwa uwanja wetu, zaidi ya kuambiwa turekebishe wigo wa
pembeni mwa uwanja baada ya mchezo kati
ya Prisons naYanga, ambao tayari turisha rekebisha haraka baada taarifa hiyo.”
Alisema Mwaluka.
Mwaluka alisema kuwa malalamiko
mbalimbali wanayopata kutoka timu
zinazoshiriki ligi kuu ni changamoto kwao na wanaendelea kuyafanyia kazi ili
kuuweka sawa uwanja huo.
Mwaluka pia alisema huduma za vyoo
uwanjani hapo kuwa ni nzuri na vipo vya
kutosha tofauti na vyombo vya habari vilivyo ripoti hivi karibuni.
“Vyoo vipo 6 ambavyo vinakizi
kabisa huduma kwa mashabaki wote
wanaongia uwanjani, “ alisema Mwaluka.
Aidha Mwaluka alisema kuwa uwanja
huo wa Sokoine unaonekana kukosa sifa ni kutokana na malekebisho makubwa waliyoyafanya
msimu huu ya kuondoa vinundu uwanjani vilivyo kuwa vinapoteza umilikaji wa
mpira kwa wachezaji.
“Tulikwetua uwanja kwa lengo la kutoa
vinundu vilivyo kuwa vinasumbua wachezaji lakini baada ya kumaliza kukwetua
kumejitokeza vishimo vidogovidogo ambavyo tunaendelea marekebisho wakati ligi
inaendelea,”alisema Mwaluka.
“Kufikia mzunguko wa pili wa ligi
kuu pichi ya uwanja itakuwa imekamilika vizuri kuliko ilivyokuwa mwanzo kabla
ya marekebisho na malalamiko hayatajitokeza tena.” alisema Mwaluka.
Wakati huo naye mmoja wa watu wanao
husika na usafi uwanjani hapo Elizabeth Mwakyoma aliwataka mashabiki wanao hudhuria uwanjani kwa ajili ya kuangalia
mpira kutumia vizur huduma ya vyoo ili kuepusha hatari ya kupata magonjwa ya
kuambukizwa, na kuwarahisishia ufanyaji wa usafi baada ya mchezo.
No comments:
Post a Comment