Sunday, October 28, 2012

CHAMA CHA MPIRA MKOANI MBEYA CHAPATA VIONGOZI WAPYA.



CHAMA cha mpira wa miguu mkoani Mbeya ( MREFA) kimepata viongozi wake katika uchaguzi  uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lungwe.

Akiongea na Hottest Newz katibu wa kamati ya uchaguzi huo Prince Mwaihojo aliwatataja walioibuka kidedea katika uchaguzi huo kuwa ni nafasi ya (Mwenyekiti)  John David Mwamwaja, (Makamu mwenyekiti) ni Omary Daud  Mkwawa Mahinya, nafasi ya (katibu) ni Seleman Haroub Said, (katibu msaidizi) ni William Wilson Mwamlima.

Mwaihojo aliwataja wengine kuwa ni wajumbe mwakilishi Taifa Oscar Donald Korosso, (mjumbe Mwakilishi vilabu) ni Juma Beblon Killa na nafasi ya (Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji) ni Dickson Lusubilo Sinkwembe, Andongwisye Ramadhan Panja na Lwitiko Edward Mwamndela.

Aidha Mwaihojo aliwashukuru wote waliofanikisha uchaguzi huo kufanyika kwa amani na kuwapongeza wote walioshinda uchaguzi huo.

Naye mwenyekiti mpya wa (MREFA) John David Mwamwaja amewataka viongozi wenzake walioshinda uchaguzi na wale walioshindwa katika kinyang’anyiro hicho kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha maendeleo ya soka katika mkoa wa Mbeya.




No comments:

Post a Comment