Monday, October 28, 2013

MAPUNDA AITWA NA KIM



KOCHA wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, amemwita kipa wa zamani wa timu hiyo, Ivo Mapunda, katika kikosi cha pili cha timu hiyo kwa ajili ya michuano ya Chalenji itakayofanyika mwezi ujao mjini Nairobi, Kenya.

Mapunda anayecheza soka ya kulipwa katika Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, anamweka nje kipa namba moja wa Taifa Stars, Juma Kasema, ambaye tangu amalize mkataba wake na Simba amekuwa hana timu ya kuchezea.

Kipa huyo ameitwa katika kikosi cha pili cha Stars kilichopewa jina la Future Young Taifa Stars, kitakachoingia kambini Novemba 9, kinachojumuisha nyota 30, wakiwamo wawili kutoka timu ngeni katika Ligi Kuu ya Bara, Mbeya City ya Mbeya, ambapo watakaofanya vizuri watapandishwa hadi kikosi cha Stars.

Nyota waliomo kwenye kikosi hicho ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars; Makipa: Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).

Mabeki: David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili na John Kabanda (Mbeya City), Himid Mao , Said Morad, Wazir Salum na Ismail Gambo (Azam), Issa Rashid, Miraji Adam (Simba), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Mohamed Hussein (Kagera Sugar).

Viungo: Amri Kiemba, Ramadhani Singano, Haruna Chanongo, Jonas Mkude na William Luccian (Simba), Farid Mussa, Khamis Mcha (Azam), , Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Simon Msuva (Yanga),

Washambuliaji: Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya na Paul Nonga (Mbeya City).

Kim alisema kuelekea mechi hiyo ya kirafiki, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Novemba 12 kabla ya siku itakayofuata kucheza na Future Young Taifa Stars kuelekea michuano ya Kombe la Chalenji.

Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa na kubaki Stars itakayoondoka Novemba 14 kwenda Arusha kwa kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayopigwa kuanzia Novemba 27 - Desemba 12.

Nyota 16 wa Taifa Stars na timu zao kwenye mabano ambao wataingia kambini Novemba 12, ni Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).

Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).

Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.


No comments:

Post a Comment