Sunday, November 3, 2013

Bonifasi Wambura Ateuliwa Kukaimu Nafasi Angetile Osiah TFF


KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF kwa vyombo vya habari leo uteuzi wa Wambura unaanzia Novemba 2 mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa kwenda likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake kwa kipindi kilichosalia. Uamuzi huo unatolewa muda mfupi tangu uongozi mpya uingie madarakani chini ya Rais wa sasa wa TFF, Jamal Malinzi.

“Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.” inafafanua taarifa iliyotolewa na Malinzi, Rais mpya wa TFF.
Hata hivyo taarifa hiyo haikufafanua zaidi sababu za kumpumzisha Osiah katika nafasi hiyo akiwa ukingoni kumalizia mkataba wake wa ajira kuitumikia TFF.

No comments:

Post a Comment