Thursday, November 14, 2013

TATIZO LA OMBA OMBA LAZIDI KUWA KERO JIJINI MBEYA

Mwenye tshirt nyeupe michirizi myesi akitoa maelezo kuhusu mtoto huyo


mtoto akiondoka eneo la chuo








Idadi ya Omba omba imezidi kuongezeka siku hadi siku hususani kwa miji mikubwa hapa Tanzania kama Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Hii imedhihirka jana jijini Mbeya mara baada ya mtoto mdogo kukutwa akiwa amejilaza maeneo ya chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (old compuss). Mahojiano mafupi yalifanyika na huyo mtoto akadai baba na mama yake walishafariki hivyo anaishi katika hali ngumu kwani hana mlezi na akidai anaumwa anahitaji msaada. Baadhi ya wanachuo walimchangia kiasi cha shilingi 5000/= na wengine wakiahidi kumnunulia chakula.
Muda mfupi alijitokeza mama mmoja akasema “yule mtoto anamfaham vizuri, na ni mwongo anaishi mitaa ya mama john na wazazi wake wote wawili ila wale wazazi wanafanya kumtumia kama chambo ili wapate hela ya kujikimu kimaisha”.
Aliendelea kwa kuwataka watu kama wana moyo wakusaidia wamsaidie tuu ila sio kwamba huyu motto hana wazazi, wazazi wake wote wawili wapo na wanaishi mama john na akadai kuna kipindi walishawahi kukamatwa na polisi wakafikishwa kituoni na kuamriwa waache tabia hiyo na wafanye kazi ile wamlee vizuri mwanao.




No comments:

Post a Comment