Saturday, November 16, 2013

Tanesco yatangaza mgao wa umeme kwa muda wa siku 10 kwenye mikoa mbalimbali na Dar ikiwemo.



Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Badra Masoud amethibitisha kuwepo kwa mgao wa umeme kwenye majiji yote matano nchini pamoja na Zanzibar na mikoa mingine kadhaa kwa siku kumi kuanzia leo na kusababisha adha kwa wakazi wake.
Badra akielezea kuwa hali hiyo inayotokana na kuzimwa kwa mitambo ya kampuni ya Pan African iliyopo Songosongo alisema,“Mitambo hiyo itazimwa kwa sababu ya matengenezo ya lazima, hakuna jinsi ya kuzuia hali hiyo Tanesco tunasikitika sana kwa kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa umeme kwenye gridi ya taifa,”.
Alifafanua mitambo hiyo inaendeshwa na gesi ambayo imepungua katika kisiwa hicho cha Songosongo Wilaya ya Kilwa, Lindi. “Upungufu huo umesababishwa na matengenezo ya kiufundi yanayofanywa kwenye visima vya gesi na lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo”.
Source : Mwananchi

No comments:

Post a Comment