Sunday, November 3, 2013

TANZANIA PRISONS WAPIGISHWA KWATA NA MAAFANDE WA JKT OLJOLO SOKOINE

Timu ya tanzania prison maarufu kama wajelajela leo wamejikuta wakiambulia kichapo cha goli 1 -0 kutoka kwa maafande wenzao wa JKT Oljolo.
Iliwachukua dakika 6 tuu maafande hao wa JKT Oljolo na kuweza kuandika goli lilodumu mpaka kipenga cha mwisho cha mwamzi kinapuliza.
Tanzania prisons itabidi wajilaumu wenyewe mara baada ya 22 kuzawadiwa penalti iliyopigwa na Jeremia juma.
Tanzania prisons mara baada ya kupoteza mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa sokoine Mbeya wameshuka mpaka nafasi ya 13 kutoka nafasi ya 12 waliyokuwepo awali.






No comments:

Post a Comment