Friday, December 21, 2012

BA IN SOCIOLOGY TEKU WAFANYA KIKAO

Mh. Tweve Nehemia akifungua kikao


Nzunda Enock akichangia hoja



moja ya wajumbe Chowo akiripoti kikaoni

Mwaipungu Asheri akichangia hoja



baadhi ya waliohudhuria wakitafakari kwa umakin, wa kwanza alie suka nywele ni Kayola Nanzige, katikati suti kijani Mwakalundwa Lusajo anefuata Njau Stephano




mh. Bikombo akiketi mara baada ya kuchangia hoja



wajumbe wakifuatilia mazungumzo hapo nyuma mwenye suti ya kijani ni Mwamwezi Edgar

mmoja wa waliochanngia hoja Siwingwa Josephat akiongea kwa msisitizo.



WANAFUNZI wa mwaka wa pili (BASO) katika chuo kikuu cha Teofilo kisanji university kilichopo nyanda za juu kusini mkoani Mbeya leo wamefanya kikao ili kujadili mambo mbali mbali katika chuo chao.



Akifungua kikao hicho mbunge wa BASO mwaka wa pili mh. Tweve Nehemia alianza kwa kuwapongeza wote waliofanikiwa kuhudhuria kikao hicho na hatimae kusoma ajenda mbalimbali. Tweve alizitaja ajenda hizo kuwa ni; mwenendo wa mfuko ulionzashwa na wanafunzi wa BASO ilikuwasaidia pale matatizo mbalimbali yanapo jitokeza, ushiriki wa wanafunzi katika shughuri za kitaaluma na mwisho namana ya kusaidiana katika taaluma na michango ya kufiwa na pongezi pale mmoja wao anapojifungua



Tweve aliwashukuru sana walio kabidhiwa dhamana ya kuhakikisha mfuko huo (TEKUBA) unaendelea vizuri mh. Paul Edward na Ng’ahara Zaina kwa kutekeleza jukumu lao ipasavyo.



Wakichangia ajenda ya ushirikiano katika suala la kitaalum wengi walionekana wakiwalaum baadhi ya wenzao kutoshiriki vyema katika kazi za makundi maarufu kama Group Assignment hali inayopelekea kuwapa kazi wenzao ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu, hoja iliyo changiwa na Siwingwa Josephat, Castory, Nzunda Enock, Bikombo Fidelis, Chiwambo Ausi, Ally Karafuu, Mandela Mselu, sun na kumaliziwa kwa msisitizo na Masunga Elikana.



Pia ajenda ya michango ya kufiwa na pongezi pale mmoja wao anapojifungua zilishika kasi huku ikiamriwa kuwa mchango utakuwa kwa atakaye fiwa tuu ndio utakuwa wa lazima na ule wa pongezi utakuwa hiari pale mtu mmoja mmoja atakapo jisikia na aina yoyote ya zawadi atakayo kuwa na uwezo nayo



Mwisho mbunge wa jimbo hilo Mh. Tweve aliahirisha kikao kwa kuwataka wanabaso kuwa na ushirikiano katika mambo mbali mbali hususani ya kiataaluma na kuwatakia sherehe njema za krismas na mwaka mpya kwa kuwataka wanaondoka salama na waludi salama.

No comments:

Post a Comment