Saturday, December 8, 2012

Bingwa wa CECAFA Tusker Chalenji Mwaka 2012 Kujulikana leo, ndugu wawili Tanzania vs zanzibar Mshindi wa Tatu.

LEO ni leo. Waswahili wanasema ‘mtoto hatumwi dukani’. Mashindano ya CECAFA Tusker Chalenji yanatarajia kumalizika leo jioni ambapo mbabe wa kombe hilo kwa mwaka 2012 atatangazwa rasmi. Timu za Taifa za Uganda na Kenya ndiyo zinazotarajiwa kucheza fainali kumpata bingwa huku timu za Tanzania, yaani Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kutoka Zanzibar zikicheza kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo. Kilimanjaro iliondolewa katika kuwania kucheza fainali baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwitu cha magoli 3-0 ndani ya dakika 90 na timu ya taifa ya Uganda. Wenzao Zanzibar waling’olewa kwenye nusu fainali kwa tabu na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars baada ya kufungwa kwa penati 6-4 baada ya kumalizika dakika 120 bila kupatikana mbabe.

No comments:

Post a Comment