Sunday, December 16, 2012

Mkutano Mkuu wa ANC Waanza Afrika Kusini

ANC yaanza mkutano wake Mkuu


CHAMA tawala cha Afrika Kusini (ANC) kimeanza mkutano wake wa taifa leo mjini Mangaung ambako chama hicho kiliundwa miaka 100 iliyopita. Katika kikao hicho chama kitachagua viongozi wake. Nje ya ukumbi wa mkutano baadhi ya wajumbe waliimba wakati wamepanga foleni kuingia ndani. Rais Jacob Zuma atapambana na naibu wake, Kgalema Motlanthe, kuania uongozi. Waandishi wa habari wanasema mkutano huo unafanywa wakati ANC inajitetea kupata imani ya wafuasi, huku chama kikizungukwa na tuhuma za rushwa kutoka serikali za mitaa hadi ofisi ya rais.

BBC

No comments:

Post a Comment