Friday, December 21, 2012

Breaking News: Lema ameshinda rufaa


MBUNGE wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema ameshinda rufaaa ya kesi yake iliyosikilizwa leo katika Mahakama ya rufaa jijini Dar es Salaam baada ya Mahakama kusema kwamba hakuna ushahidi wowote katika kumbukumbu ya Mahakama kama waliofungua kesi hiyo walikuwa wapigakura.

Mahakama hiyo pia imesema kwamba hata kama wangekuwa wapigakura hawana haki ya kufungua kesi hiyo kisheria huku wakitakiwa kulipia gaharama za kuendesha rufaa hiyo.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa Mahakamani hapo, wafuasi wa Chadema walifulika ndani na nje ya mahakama hiyo, hata hivyo baada ya Lema kutangazwa mshindi wa rufaa hiyo ukumbi wa mahakama ililipuka kwa kwa shangwe ikifuatiwa na msafara wa Chama hicho kwenda katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni.

No comments:

Post a Comment