Sunday, December 16, 2012

WANAMAKAMBAKO WAMWITA DEO FILIKUNJOMBE 'JEMBE'

na francis godwin Njombe

]MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara Philip Mangula. Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala. Hivyo alisema kuwa imani ya wana CCM kwa safu ya sasa chini ya mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete katibu mkuu Abdalaman Kinana na makamu mwenyekiti wa bara Mangula na makamu wake wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein na viongozi wengine ndani ya CCM ni matumaini mapya kwa wana CCM na tishio kwa vyama vya upinzani. " Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe . Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.  

No comments:

Post a Comment