Saturday, December 8, 2012

ZANZIBAR HEROES WAFANYA KWELI, WAICHABANGA KILL STARS.

TIMU ya mpira wa miguu ya Zanzibar Heroes kutoka mjini Zanzibar imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika mashindano ya CECAFA Tusker Chalenji baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars mabao 6-5. Zanzibar imeifunga Kili Stars ya Tanzania bara baada ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kumalizika dakika 90 huku timu zote zikiwa sare ya 1-1. Ndipo mpambano huo ukaariwa zipigwe penati kumpata mshindi wa nafasi ya tatu. Muda wowote kuanzia sasa itaanza fainali yenyewe kati ya Timu za Taifa za Kenya na wenyeji Uganda.

No comments:

Post a Comment