Saturday, December 8, 2012

Kandoro amewataka waislamu kushirikiana na kujenga umoja miongoni mwao badala ya kutengeneza majungu ambayo yanaathiri maendeleo yao.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na waislam wa sokomatola katika uzinduzi wa mfuko wa maendeleo mkoa wa Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka waislamu kushirikiana na kujenga umoja miongoni mwao badala ya kutengeneza majungu ambayo yanaathiri maendeleo yao. Bw. Kandoro alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mfuko wa Maendeleo cha mkoa wa Mbeya MRIDEF kilichopo Sokomatola jijini Mbeya leo asubuhi. Alisema kuwa waislamu wamekuwa hawana kawaida ya kujituma katika maendeleo hali ambayo inachangia kwa asilimia kubwa kurudisha maendeleo hivyo aliwataka kujikita katika kazi katika maeneo yao ili kuepuka malalamiko ya kutengwa katika shughuli za maendeleo. '' Jishughulisheni kwenye kazi za maendeleo na ujasiriamali, tusome elimu zote za dini na dunia, tuwasomeshe watoto wetu wapate elimu zote za dunia na akhera''alisisitiza Bw. Kandoro. Alisema kila mzazi aangalie fursa zinazomzunguka ili ajijengee uchumi katika kaya yake na kumudu huduma za msingi na kujiongezea kipato halali. Kwa upande wake Katibu wa mfuko wa Maendeleo ya Waislamu Mkoa wa Mbeya Shekhe Abbas Mshauri alisema kuwa madhumuni ya Taasisi hiyo ni kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kidini na kuongeza elimu na uchumi wa kila mmoja kulingana na maadili ya Uislamu. Alisema kuwa taasisi imedhamiria kuweka vitega uchumi na mahusiano na ushirikiano na asasi zingine za kidini Kitaifa na Kimataifa.

No comments:

Post a Comment