Monday, October 29, 2012

Boris Bunjak atupiwa virago Azam FC





Klabu ya Azam FC imeamua kumtupia virago kocha wake mserbia Boris Bunjak.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom zinasema kwamba kocha huyo ametimuliwa rasmi kukinoa kikosi hicho cha wanalambalamba.

Ikumbukwe kuwa mserbia huyo alisaini mkataba wa miaka 2 kuifundisha klabu hiyo, mara baada ya kocha Stewart Hall kutimuliwa.

Habari kutoka ndani ya klabu hoyo zinasema viongozi wapo katika mchakato wa kumrudisha kocha wao wa zamani muingereza Stewart Hall  ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Sofa paka ya Kenya.

Hatua ya kumtupia virago kocha Boris Bunjak imekuja mara baada ya Azam FC kuambulia kichapo cha 3 – 0 kutoka kwa vinara wa ligi kuu Simba Sports Club.

No comments:

Post a Comment