Monday, October 15, 2012

Tanzania Prisons Hoi

kittaaki.blogspot.com
Hiki ni kikosi cha maafande wa Jkt Oljoro


wachezaji wa Tanzania Prisons 

nahodha wa Tanzania Prisons na wa Jkt Oljoro wakipeana mikono na waamzi 


Na haya ni baadhi ya matukio ya uwanjani kwa upande wa watazamaji






Tanzania Prisons hoi Sokoine.

Wimbi la kutofanya vizuri kwa Wajelajela Tanzania Prisons limeendelea kuiandama katika uwanja wao wa nyumbani Sokoine ni baada ya jana kuangukia pua dhidi ya Maafande wenzao wa JKT Oljoro kwa jumla ya goli 1-0,

Katika pambano hilo iliwachukua dakika tano Oljoro kuandika goli lililofungwa kiufundi na Amir Omar baada ya kuunganisha kros safi iliyopigwa kutoka winga ya kulia na kumkuta mfungaji wa goli hilo pekee.

Katika pambano hilo Prisons itabidi ijilaamu yenyewe kwa kukosa magol mengi ya wazi katika dakika za 15, 34, 38, 60 na 85 kupitia kwa washambuliaji wake.

Baada ya mechi hiyo Kocha Mkuu wa Prisons Jumanne Charlse alitoa lawama kwa washambuliaji wake kwa kukosa umakini uliosababisha kukosa mgoli mengi ya wazi,

Tanzania Prisons mpaka sasa wamefanikiwa kupata pointi 3 tu na kufunga goli 1 kati ya michezo minne iliyofanyika katika uwanja wao wa  nyumbani.
Kwa upande mwingine mashabiki wa soka jijini Mbeya walikasirishwa sana na mwenendo wa timu yao katika mechi zinazofanyika katika uwanja wao wa nyumbani.

Pamoja na kipigo hicho Tanzania Prisons jumatano ya wiki hii watakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya timu ngumu ya Azam FC ,maarufu kama Wanalambalamba kutoka Dar es Salaam ambao wanashikilia nafas ya pili katika mwendelezo wa ligi kuu .



No comments:

Post a Comment