Sunday, October 21, 2012

Ingoma inogile sokoine, wajelajela waua.



Kocha wa Tanzania Prisons Jumanne Chale akiwaongoza vijana wake kwenda  kwenye vyumba vya kubadilishia nguo

Tanzania p wakifanya warm up kujiandaa kuingia uwanjani.

Toto African wakinyosha misuli kujiandaa kuingia uwanjani.

Lugano Mwangama jezi nyeupe nahodha wa tz p. na nahodha wa  Toto African wakiwa na waamuzi .

Mchezo ulimalizika kwa wajelajela tanzania Prisons kuwatandika Toto African gori 1 - 0. Gori hilo lilipatikana kunako dakika ya 33 ya mchezo kupitia kwa kiungo wao machachali Peter Michael akiunganisha kona safi iliyochongwa na Henry mwalugala kutoka magharibi mwa uwanja.

Baaada ya hapo vijana wa Tanzania Prisons waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao kama nyuki huku wakiwatumia washambuliaji wao wa pembeni Augustino Tino, John Matei na Misango Magai.

Kipndi cha pili kilianza kwa Toto African kuzinduka na kufika mara kadhaa langoni mwa wapinzani wao kupitia kwa washambuliaji wao Emaanuel Swita, Seleman Kiputa na Kheri Mohamed, lakini uimara wa kipa na safu yote ya ulinzi ya Prison ilikuwa kikwazo kwao kupata gori la kusawazisha kwani mpaka mwamuzi Simon Mbelwa kutoka pwani anapuliza kipenga chake cha mwisho matokeo haya kubadilika.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa timu ya Tanzania Prisons katika uwanja wake wa nyumbani, na kwa ushindi huo Tanzania  Prisons imekwea mpaka nafasi ya sita kwa kujikusanyia jumla ya pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara 9. Uhindi huo umepokelewa kwa shangwe kubwa na wadau pamoja na mashsbiki wa soka Jijini Mbeya.

Katika viwanja vingine mzimu wa sare umeendelea kuiandama timu ya Simba baada ya kutoshana nguvu na Mgambo Jkt huko Mkwakwani, Jkt Oljolo 1-1 na  Jkt Ruvu katika uwanja wa chamazi.



No comments:

Post a Comment