Tuesday, October 30, 2012

MH. BENARD MEMBE ATEMBELEA MPAKA WA TZ NA MALAWI NA KUONGEA NA WAZEE KYELA(MBY)




waziri Membe akiaangalia mpaka wa Tz  na  Malawi

kamati ya ulinzi na usalama wakimsikiliza waziri


mkuu wa wilaya ya kyela Mhe. M. Malenga

Waziri na kamati yake mpakani


mkuu wa wilaya ya Kyela akimuongoza waziri kuelekea mpakani

ziwa nyasa

waziri Membe

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mzozo kuhusiana na mpaka kati ya tanzania na malawi hali ambyo imelekea sintofahamu miongoni mwa watanzania waliowengi hususani wale wanaoishi mpakani.


Kufuatia hali hiyo waziri wa mambo ya nje na ushirikiaona wa kimataifa wa tanzania mh. Benard Membe amefanya ziara mkoani Mbeya na kuenda moja kwa moja wilani kyela na kwenda kujionea kinachoendelea huko.

Membe alifanikiwa kuongea na wazee wakazi wa huko mpakani ambapo alianza kwa kuwatoa hofu wazee hao kwa kuwaambia kuwa wasiwe n wasiwasi watakuwa salama na waendelee kutumia maji ya ziwa nyasa kwani ni halali yao na ni rasilimali waliyopewa na mwenyezi mungu wala hakuna mtu alichimba ziwa hilo.

Membe alianza kwa kutoa historia fupi anayoifahamu kuhusiana na mpaka huo, na baadae wazee mbalimbali wakazi wa hapo walipata fursa ya kutoa historia wanayoifahamu.




Wakiongea kwa nyakati tofauti wazee hao waliweza kutoa historia mbalimbali kuhusu mpaka huo na kutoa mambo mengine ambayo hata Mh. Membe alibaki kushangaa kwani hajawahi kusikia, hali ambayo ilimpelekea waziri kuwasikiliza kwa umakini.

"Hao wameshindwa ya kuongea kuhusiana na mpaka huu kwani hata hivi kuna makaburi ya babu na bibi zetu yamekwisha mezwa na ziwa, kuanzia hapa tulipo ni km kazaa kwenda mbele ndipo mpaka ulikuwa kipindi cha utawala wa Mjerumani na kithibitisho ni kwamba yule Mjerumani kuna mibuyu ipo kule iligongwa mihuri miwili isiyofutika ikisomemeka Tanganyika territory paka leo ipo.

Akaendelea kwa kusema kuna kitabu kilichotolewa kipindi cha Mjerumani wa kwanza ambaye alikuja kuleta dini ya Moravian ukurasa wa 13 kinaelezea vizuri kuhusu mpaka huu, akatoa kitabu". Mzee

Hata hivyo waziri kwa heshima na taadhima alimumba huyo mzee hicho kitabu kama ushahidi na akaahidi kukirudisha mara baada ya kukifanyia kazi.

Akihitimisha waziri aliwashukuru wote waliohusika na kuwataka kuwa na amani na kuendelea na shughuli za kiuchumi kama kawaida.

"Tutaenda Ujerumani, Uingereza na Addis Ababa nchini Ethiopia yaliko makao makuu ya umoja wa kimataifa ilikupata vielelezo vya kutosha" alisema Membe.




No comments:

Post a Comment