Monday, October 22, 2012

Godfrey Bonny Mwandanje arudi kuiongezea Mbeya City nguvu.




TIMU ya soka ya Mbeya City ya jijini Mbeya inayoshiriki ligi daraja la kwanza Taifa imetamba kufanya vizuri katika mashindano hayo na kupanda daraja ili kucheza ligi kuu Tanzania bara katika msimu ujao.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalwis aliiambia Hottest newz kuwa mwaka huu hawatakubali tena kukosa nafasi ya kucheza mashindano ya Ligi kuu mwakani kutokana na jinsi walivyo jipanga.

Alisema maandalizi yao yako vizuri na wako tayari  kupigana mpaka dakika ya mwisho ili waweze kufuzu fainali na kufanikiwa kuwa miongoni mwa timu zitakazo panda daraja msimu huu.

Mwalis alisema ili kufanikisha lengo lao la kupanda daraja wameawasajili baadhi ya wachezaji wazoefu akiwamo Godfrey Bonny Mwandanje ambao watawasaidia katika harakati za kufanya vizuri.

“Tumejipanga sana hatutafanya makosa kama msimu uliopita , tumerekebisha makosa mbalimbali yaliyotufanya tukashindwa kupanda daraja licha ya kuwa tulianza vizuri lakini msimu huu tutaanza kwa kasi na kumaliza vizuri” alisema Mwalis.

Alisema licha ya timu nyingi kujiaandaa sana na ugumu wenyewe wa ligi daraja la kwanza, lakini kikosi chao kimepata muda mwingi wa kujiandaa na kufanya marekebisho yaliyo jitokeza msimu ulio pita.

Aidha Mwalwis alisema kuwa timu yake imepangwa katika kundi A, pamoja na timu za Majimaji ya Songea, Bukinafaso ya Morogoro , Kurugenzi ya Mufindi, Small kids ya Sumbawanga, Mlale ya Ruvuma, Polis ya Iringa na Mkamba ya Morogoro.

Ligi hiyo ya daraja la kwanza inatarajia kuanza juma tano  ambapo Mbeya City itakuwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakikaribishwa na wenyeji Bukina Faso ya mjini hapo.







No comments:

Post a Comment