Friday, October 19, 2012

Meneja wa uwanja wa Sokoine akanusha kufungiwa kwa uwanja

uwanja wa sokoine mbeya.






MENEJA Modestus Mwaluka wa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambao unatumiwa  na timu ya Tanzania Prisons kama Uwanja wa nyumbani amekanusha taarifa ya vyombo vya habari kuwa upo hatarini kufungiwa na TFF  kutokana na ubovu.
                           
Uwanja wa huo hivi karibuni umekuwa ukilalamikiwa na baadhi ya timu ambazo hushuka katika mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara kuwa pichi yake ni mbaya na haufai kutumika kwa mashindano ya ligi.

Akizungumza na Hottest newz jana Mwaluka alikanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya habari nchini kuwa uwanja huo upo hatarini kufungiwa na Shirikisho linalo simamia mpira wa miguu TFF.

“Hatujapata taarifa zozote kutoka TFF za kuhusu kufungiwa uwanja wetu, zaidi ya kuambiwa turekebishe wigo wa pembeni mwa  uwanja baada ya mchezo kati ya Prisons naYanga, ambao tayari turisha rekebisha haraka baada taarifa hiyo.” Alisema Mwaluka.

Mwaluka alisema kuwa malalamiko mbalimbali wanayopata kutoka  timu zinazoshiriki ligi kuu ni changamoto kwao na wanaendelea kuyafanyia kazi ili kuuweka sawa uwanja huo.

Mwaluka pia alisema huduma za vyoo uwanjani hapo kuwa ni nzuri na vipo vya   kutosha tofauti na vyombo vya habari vilivyo ripoti hivi karibuni.

“Vyoo vipo 6 ambavyo vinakizi kabisa  huduma kwa mashabaki wote wanaongia uwanjani, “ alisema Mwaluka.

Aidha Mwaluka alisema kuwa uwanja huo wa Sokoine unaonekana kukosa sifa ni kutokana na malekebisho makubwa waliyoyafanya msimu huu ya kuondoa vinundu uwanjani vilivyo kuwa vinapoteza umilikaji wa mpira kwa wachezaji.

“Tulikwetua uwanja kwa lengo la kutoa vinundu vilivyo kuwa vinasumbua wachezaji lakini baada ya kumaliza kukwetua kumejitokeza vishimo vidogovidogo ambavyo tunaendelea marekebisho wakati ligi inaendelea,”alisema Mwaluka.

“Kufikia mzunguko wa pili wa ligi kuu pichi ya uwanja itakuwa imekamilika vizuri kuliko ilivyokuwa mwanzo kabla ya marekebisho na malalamiko hayatajitokeza tena.” alisema Mwaluka.

Wakati huo naye mmoja wa watu wanao husika na usafi uwanjani hapo Elizabeth Mwakyoma aliwataka mashabiki  wanao hudhuria uwanjani kwa ajili ya kuangalia mpira kutumia vizur huduma ya vyoo ili kuepusha hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa, na kuwarahisishia ufanyaji wa usafi baada ya mchezo.







No comments:

Post a Comment