Monday, October 15, 2012

SOKOINE HATARINI KUFUNGIWA

SOKOINE HATARINI KUFUNGIWA

KOCHA Mkuu wa timu ya JKT Oljoro ya Arusha inayo shiriki michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara Mbwana Makata amesema ubaya wa pichi ya uwanja wa Sokoine Mbeya unawokosesha wakazi wa Mbeya kupata burudani nzuri.


Makata alitoa kauli hiyo juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.



Alisema uwanja wa Sokoine ni moja kati ya viwanja ambavyo pichi yake ni mbaya wala  haufai kuchezea mashindano makubwa kama ligi kuu.



“Kutokana na ubaya wa  pichi ya uwanja  unawafanya wakazi wa Mbeya wapenda soka kushindwa kupata burudani kutoka kwa timu mbalimbali zinazo fika katika uwanja huu kwa sababu huzilazimu timu kubutua butua mpira” alisema Makata.



Makata alisema licha ya timu yake kuibuka na ushindi lakini walishindwa kuwaonyesha kandanda safi wakazi wa Mbeya kutokana na uwanja huo kuwa mbaya ukilinganisha na viwanja vingine vinavyotumika kwa mashindano ya ligi kuu.



Makata ambaye amewahi kuifundisha Prisons pia  aliwataka wahusika  kurekebisha haraka pichi ya uwanja ili wadau na washabiki wa mpira waweze kupata burudani wanayo ikosa kwa sasa katika uwanja huo.



Aidha alifurahishwa na ushindi wa goli 1-0 ugenini na kusema kuwa sasa wamejipanga kufanya vizuri kwa mechi dhidi ya Afrika Lyon utakaofanyika Arusha juma tano.



Kwa upande mwingine mashabiki wa soka jijini Mbeya wamechukizwa na mwenendo mbaya wa timu yao katika mechi za nyumbani kwani mpaka sasa wameaambulia pointi 3 tu na goli moja  kati ya mechi 4 walizo cheza katika uwanja wao wa Sokoine.


















No comments:

Post a Comment